BILIONEA NAMBA MOJA DUNIANI AIMWAGIA SIFA TANZANIA

Tajiri namba moja dunia, Bill Gates jana alijiunga rasmi katika mtandao wa kushirikishana picha wa Instagram akiwa nchini Tanzania ambapo picha zake tatu za kwanza alizoweka, ni alizopiga akiwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kicheba iliyopo wilayani Muheza, mkoani Tanga.
Katika mtandao huo, Bill Gates ambaye ni Mwenyekiti Mwenza wa Taasisi ya Bill and Mellinda Gates anatumia jina la “thisisbillgates” kwa sababu jina la “billgates” tayari linatumiwa na mtu mwinngine.
Gates aliisifia Tanzania na akieleza namna alivyofurahishwa na kukutana na mtaalamu, Upendo Mwingira aliyejitolea maisha yake kwa ajili ya kupambana na magonjwa yasiyopewa kipaumbele.
Mimi (Bill Gates) na Melinda tumekuwa tukija Tanzania kwa miaka mingi sasa. Huwa nafurahishwa kuona hatua ambazo nchi hii imepiga katika kuboresha huduma za afya pamoja na kutoa fursa.
Aidha, Gates alisifia mazingira ya Tanzania huku akisema kila mara anaposafiri kwenye eneo kama hili, anatamani pia watu wengine nao waje waweze kukutana na watu ambao huwa nakutana nao. Sina mashaka kuwa nitawaacha wakiwa na matumaini kama nilivyonayo mimi kuhusu maendeleo yanayotokeo kote ulimwenguni.
Nitakuwa nikiwashirikisha picha za safari zangu kupitia Instagram, na ninaamini mtafuatana nami, aliandika Bilione huyo.


Kwa mujibu wa jarida la Forbes, Gates utajiri wake unakadiriwa kuwa dola za kimarekani 89.5 bilioni (Tsh 200.5 trilioni) ambazo hazijumuishi dola za kimarekani 31.1 ( Tsh 70 trilioni) ambazo huzitoa kama misaada kwa jamii.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post