BREAKING: MATOKEO YA KURA YA KUTOKUWA NA IMANI NA RAIS ZUMA YATANGAZWA

Rais wa Afrika Kusini anusurika kwa mara nyingine katika kura ya kutokuwa na imani naye iliyopigwa na bunge la nchi hiyo ambapo awamu hii ilikuwa ni ya tofauti kwani ilikuwa ni kura ya siri.
Rais Zuma kwa vipindi vya mfululizo ameshuhudia maandamano na kura za kutokuwa na imani zikipigwa kwa lengo la kumtaka ajiuzulu kutokana na tuhuma mbalimbali za rushwa na upendeleo zinazomkabili.
Kutokana na kura zilizopigwa leo na bunge la nchi hiyo, jumla ya kura hizo ni 384 huku waliosema hawana imani naye wakiwa 177, wenye imani wakiwa ni 198 na kura zilizoharibika ni 9.
Kwa mujibu wa matokeo hayo, Wabunge 40 wa chama tawala, ANC wamepiga kura ya kutokuwa na imani na Rais Jacob Zuma hivyo kutaka ang’atuke.
Viongozi mbalimbali wa ANC pamoja na wabunge wengine wa chama hicho, wametaka wabunge hao (40) wachukuliwe hatua za kinidhamu kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kukisaliti chama.
Muda mfupi baada ya bunge kutangaza matokeo hayo yaliyokuwa yakisubiriwa kwa hamu, wafuasi wa Rais Zuma wameonekana wakicheza na kuimba kwa furaha nje ya jengo la bunge wakisherehea ushindi huo.
Aidha, kwa upande mwingine imeripotiwa kuwa, fedha ya Afrika Kusini (Rand) imeporomoka kwa zaidi ya asilimia 1 baada ya kutangazwa kuwa Rais Zuma ameshinda kwenye kura hiyo.
ANC imempongeza Rais Zuma kufuatia ushindi huo huku kikisema kwamba, mara zote kimekuwa kikitoa makada wenye kuaminika katika nafasi za serikali.
Chama tawala cha Afrika Kusini, ANC kimempongeza Rais Zuma kufuatia ushindi katika kura ya kutokuwa na imani iliyopigwa leo. 


Rais Zuma amepigiwa kura ya kutokuwa na imani naye kwa zaidi ya mara 5 ambapo mara zote amefanikiwa kuruka kiunzi na kuendelea kusalia madarakani.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post