CHID BENZ AKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA

Ikiwa kumbukumbu za namna alivyoteseka kutokana na matumizi ya dawa za kulevya zikiwa hazijafutika vichwani mwa watu wengi, mwanamuziki Chid Benzi  amekamatwa tena na dawa za kulevya.
Watu saba akiwemo Chid Benz ambaye jina lake halisi ni Rashid Makwiro wamekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Ilala kufuatia msako uliofanyika ambapo wamekutwa na dawa za kulevya aina ya heroine.
Hivi karibuni tu Chid Benz alikuwa ameanza kurejea katika kazi zake za kisanii ambapo alitoa wimbo wa Q Cheif akielezea mateso aliyopitia huku wengi wakiamini kuwa ameacha matumizi ya dawa hizo.
Aidha, amekuwa akishiriki matamasha mbalimbali ya muziki na afya yake ilianza kuonekana imeimarika, wengi wakifurahishwa na maendeleo hayo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni amesema watuhumiwa hao walikamatwa Agosti 12 majira ya saa 11.50 jioni wakijihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya.
“Chid Benz na wenzake wapo kituo cha Polisi cha msimbazi ambapo tunaendelea na upelelezi ukikamilika tutawafikisha mahakamani na kiasi cha dawa zilizokamatwa zimepelekwa kwa mkemia mkuu na itajulikana ni kiasi gani za dawa za kulevya zilizokamatwa,”amesema Hamduni.
Kamanda huyo alisema kwa baada ya kuwakamata vijana hao sasa wanajikita kusaka mtandao mzima unaohusika na biashara hiyo ili kuhakikisha hatua kali zinachukuliwa dhidi yao.
Hii si mara ya kwanza kwa msanii huyo kukamatwa na dawa za kulevya kwani Oktoba 24,2014, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jiji la Dar es Salaam alikamatwa akiwa na dawa za kulevya, akijaribu kupita nazo kwenda mkoani Mbeya kwenye tamasha la muziki.
Chid Benz alinusurika kufungwa baada ya kufanikiwa kulipa faini ya Tsh 900,000 na mahakama ikamuachia huru.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post