CUF WAIPONGEZA SERIKALI KUFUTA UMILIKI WA SHAMBA LA MKE WA SUMAYE

Chama cha Wananchi (CUF) kimeipongeza serikali kufuta umiliki wa shamba la Mke wa Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye lakini wakisisitiza kwamba ujasiri huo huo utumike kuyatwaa mashamba ya vigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambayo nayo hayajaendelezwa.
Mwenyekiti wa CUF Mkoa wa Morogoro, Abeid Mlapakolo aliliambia gazeti la Mwananchi kuwa, kuna vigogo wengi wa CCM wanaomiliki mashamba mkoani humo ambayo hayajaendelezwa.
Kwa kuwa serikali imeonyesha ujasiri wa kuchukua shamba la Esther Sumaye, basi wangefanya hivyo hivyo kwa vigogo wengine ambao nao wanamiliki mashamba kama yake.
Kiongozi huyo alisema kuwa suala la ukaguzi na uwasilishaji wa orodha ya mashamba pori yanayotakiwa kubatilishwa mmiliki halifanyiki kwa uwazi na kwamba kuna mengine yanastahili kufutiwa lakini hilo halifanyiki kutokana na majina makubwa ya wamiliki.
“Kwa muda mrefu serikali imetengeneza migogoro kwenye vijiji vyetu kwa kukumbatia watu hawa na kuwasababisha wananchi kukosa maeneo ya kilimo na pia kuchangia migogoro ya wakulima na wafugaji kwa kugombea maeneo madogo yaliyopo kwa kilimo.”
Mlapakolo alisema kwamba, watu pekee wenye uwezo wa kumiliki mashamba makubwa wasiyaendeleze na bado wasinyang’anywe ni wanaCCM.
Kwa upande wake Kamishna Msaidizi  wa Ardhi Kanda ya Mashariki, Juliana Pilla alisema ubatilishaji wowote wa ardhi unafuata sheria, kanuni na taratibu ambazo zinamtaka mmiliki wa shamba ndani ya miaka 5 tangu kumilikishwa shamba awe ameendeleza tano ya nane ya eneo alilomilikishwa kisheria.
Alisema kuwa, kabla ya kuchukua hatua ya kufuta umiliki wa shamba pori, huwa wanajiridhisha kwa kufanya ukaguzi na kutoa notisi inayomtaka mmiliki kuendeleza shamba, ana asipofanya hivyo ndipo hatua za ubatilishaji umiliki hufuata.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post