DARASA LA SABA WAMZUIA LEMA KUFANYA MIKUTANO JIMBO KWAKE

Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amezuiwa kufanya mikutano ya hadhara jimboni kwake kati ya leo (Agosti 27, 2017) hadi Septemba 8, 2017 ili kupisha shughuli mbili zinazotakiwa kufanyika mkoani humo.
Katika barua iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, na kusainiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo imeeleza kuwa ombi la mbunge huyo la kutaka kufanya mikutano limezuiwa, kwanza kwa sababu ya maandalizi ya mitihani ya darasa la saba lakini pili, maandalizi ya ujio wa mwenge wa uhuru.
Zuio hilo lilinukuu barua ya tarehe 23/8/2017 ya mbunge hiyo iliyokuwa ikitoa taarifa za mkutano wa hadhara.
“Ofisi ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha inakutaarifu kuwa imezuia mikutano yako yenye ratiba ya 27/8/2017 hadi 1/9/2017 kwa sababu zifuatazo;”
“Maandalizi ya kuhitimisha mitihani ya darasa la saba na mwenge wa uhuru ambayo ni matukio makubwa ya kitaifa kwa tarehe hizo. Baadhi ya viwanja vilivyopo kwenye ratiba yako ya mikutano navyo vipo kwenye maandalizi kwa ajili ya moja wapo ya matukio hayo.”
Aidha, Polisi wamemueleza mbunge huyo kuwa, kutokana na sababu hizo anaweza kupanga mkutano muda wowote baada ya kumalizika kwa mitihani ya darasa la saba yaani Septemba 8.
Kamanda wa Polisi alisema pia, Polisi wanahitajika katika maaandalizi ya mwenge na mitihani hiyo, hivyo hawawezi kupata Polisi wa kutosha kugawanywa sehemu zote hizo tatu.
Kwa upande wake, Lema amepinga sababu zote zilizotolewa na Polisi na kusema kuzuiwa kwa mikutano yake ni njama za kisiasa kwani kwenye mikutano 10 aliyofanya imekuwa ya mafanikio makubwa, wananchi wamemuunga mkono na pia wamepata nafasi ya kufahamu ukweli wa mambo mbalimbali.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post