DIAMOND AMEIBA WIMBO MATONYA? MWENYE WIMBO AFUNGUKA

Mwanamuziki Seif Shaban maarufu kwa jina lake la sanaa, Matonya amelalamika WCB wakiongozwa  na mwanamuziki Diamond Platnumz kutumia vionjo vya wimbo wake wa Zilipendwa bila idhini yake.
Malalamiko hayo ya Matonya yamekuja ikiwa ni saa chache tu tangu Diamond na kundi lake walipoachia video ya wimbo wao ambao unaitwa Zilipendwa unaochambua matukio na watu waliokuwa maarufu miaka ya nyuma lakini kwa sasa wamesahaulika au vimesahaulika.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Matonya amesema kwamba, kwanini imekuwa vigumu kwa WCB kumpa taarifa kama walivyofanya kwa Saida Carol walipotumia wimbo wa Salome?
“Nduguzangu wasafi / Nawapongeza sana kwa kazi mzuri mnazo zifanya / Nilifurahi Sana mlichokifanya kwa saida karoli dadaetu/ mlimuita mkamshirikisha akawapa Baraka zake/ kwangu mlishindwa nini?.”
Matonya amefafanua kwamba, yeye hakuwa na uhitaji wa fedha kama inavyoweza kudhaniwa, la hasha lakini alitaka tu heshima ya kwamba umetambua thamani yake kwa kuamua kutumia kazi yake.
“Sina shida Ya Pesa nina shida Ya heshima cose najua dunia ni mapito,” ameandika Matonya.
Matonya ambaye ni miongoni mwa wasanii wenye mchango mkubwa katika muziki wa Tanzania, amesema kuwa, kama yeye anafanyiwa hivi, vipi kuhusu wasanii wanaochipukia ambao hawana sauti na hawafahamiki kwenye jamii?
“Kama mimi naibiwa haki yangu vipi wasanii wachanga? Basata mkowapi? Wadau Wa muziki mkowapi? Usipo ziba ufa tajenga kuta!!.”
Aidha amesema kwamba anaamini haki yake itapatikana.
Wakati huo huo, Afande Sele ambaye naye ametajwa kwenye wimbo huo mpya wa WCB kuwa ni Zilipendwa, amesema hana tatizo na kitendo hicho na kwamba ni sehemu ya sanaa na watu huja na kupita.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post