DIWANI WA CCM AKAMATWA KWA KUJIFANYA USALAMA WA TIAFA

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha linamshikilia Diwani wa Kata ya Sambasha, Lengai Ole Sabaya (CCM) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Arusha kwa tuhuma za kujifanya Ofisa wa Usalama wa Taifa.
Akizungumza, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema wamemkamata kiongozi huyo kutokana na tuhuma hizo ambazo alizitenda kipindi cha nyuma na amewahi kufikishwa mahakamani lakini shauri hilo likafutwa.
Akizungumzia sababu za kuondolewa mahakamani kwa shtaka hilo la awali, Mkumbo alisema kwamba walifanya hivyo ili kuweza kukamilisha uchunguzi ambao kwa sasa umekamilika na hati ya mashtaka ipo tayari.
“Kosa lake ni kuwa alijifanya yeye ni Ofisa wa Usalama wa Taifa (TISS) wakati sio kweli. Kwa kuwa suala la upelelezi ni la kitaalamu ndiyo sababu tukaiondoa kwanza. Hao wanaosema amekamatwa kwa sababu za kisiasa si kweli kwani sisi si wanasiasa, na tunafanya kazi kwa mujibu wa sheria.”
Mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani la asubuhi kusomewa shtaka linalomkabili.
Aprili 28 mwaka huu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ilimuachia huru Ole Sabaya baada ya kuifuta kesi iliyokuwa ikimkabili baada ya upande wa mashtaka kushindwa kupeleka ushahidi mahakamani. Aliyekuwa wakili wa serikali katika kesi hiyo, Grace Madikenya aliiomba mahakama kuiondoa kesi hiyo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post