ESTHER SUMAYE YAMKUTA SAWA NA YA MUMEWE, FREDERICK SUMAYE

Serikali imefuta umiliki wa shamba la ekari 473, lililokuwa linamilikiwa na Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, Esther Sumaye na mengine manne ya ekari 2,661 ya Kampuni ya Noble Agriculture Enterprises Limited, inayomilikiwa na mfanyabiashara Jeetu Patel baada ya kushindwa kulipia kodi ya ardhi na kutoyaendeleza.
Huo ulikuwa ni muendelezo wa serikali kuyatwaa mashamba ambayo wamiliki wake kwa muda wameshindwa kuyaendeleza au kulipia kodi.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ilieleza kuwa Rais Magufuli amefuta mashamba pori 14 yenye ukubwa wa zaidi ya ekari 14,341 katika wilaya za Kilosa, Mvomero na Kilombero mkoani Morogoro. Mashamba ya Esther Sumaye na Patel ni miongoni mwa mashamba hayo yaliyofutwa na Rais.
Baada ya kufuta mashamba hayo, Waziri William Lukuvi alisema kuwa Rais amewaagiza Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya kuhakikisha mashamba hayo yanasimamiwa vizuri na kugawiwa kwa wananchi hasa wenye uhitaji ambao wapo jirani na mashamba hayo.
Pamoja na mambo mengine, Waziri Lukuvi amewaonya viongozi wenye nia ya kujipenyeza kwa lengo la kuchukua maeneo kwenye mashamba hayo na kwamba wale watakaojipenyeza watajulikana na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk. Stephen Kebwe alisema kuwa awali serikali ya mkoa ilifanya uchunguzi na kubaini uwepo wa mashamba pori 223 huku Wilaya ya Kilosa ikiongoza kwa kuwa na mashamba 198.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post