FAHAMU AINA NA MATUMIZI YA TAA MBALIMBALI ZA KWENYE GARI

SHARE:

Taa katika gari lako unaweza kuona ni kitu kinachotumika tu kukupatia mwanga, lakini kiukweli, taa katika gari ni muhimu kwani zinafanya ...

Taa katika gari lako unaweza kuona ni kitu kinachotumika tu kukupatia mwanga, lakini kiukweli, taa katika gari ni muhimu kwani zinafanya kazi mbalimbali zaidi ya ile ya kutoa mwanga kama vile kutoa ishara ya muelekeo wa gari, hali ya gari na zaidi.
Unaweza kujikuta unatozwa faini kila mara, ukafungwa gerezani au kupata ulemavu na hata kifo (kutokana na ajali) endapo utashindwa kutumia kwa usahihi taa za gari lako.
Japokuwa inaweza kuonekana ni kitu kidogo na cha kawaida, lakini baadhi ya madereva hukumbwa na wakati mgumu kujua aina sahihi ya taa za kutumia katika eneo husika. Wengine hawafahamu hata aina mbalimbali za taa zilizopo katika gari, wengi wao wanajua taa za kumulika barabarani tu.
Katika makala ya leo, tutachambua aina mbalimbali za taa kwenye gari na matumizi yake.
Taa za mbele
Kuna aina mbili za taa za mbele, taa zenye mwanga mdogo (Low beam lights) na taa zenye mwanga mkali (High beam lights).
Mwanga wa taa hizi humsaidia dereva kuona barabara vizuri wakati wa usiku lakini pia huwawezesha madereva na watumiaji wengine wa barabara kujua kuwa kuna gari linakuja.
Taa zenye mwanga mdogo hukuwezesha kuiona barabara na haiwaathiri madereva au watumiaji wengine wa barabara kutokana na kiwango kidogo cha mwanga wake. Wakati mwingine taa hizi hutumika hata mchana endapo kuna ukungu mkali ili kutoa ishara kwa watumiaji wengine wa barabara.
Image result for Low beam car lights gif
Unaweza kutumia taa zenye mwanga mkali endapo hakuna gari jingine au chombo kingine cha moto kinachokuja mbele yako. Kutokana na mwanga huo mkali, ukimpiga machoni dereva mwingine anaweza kupoteza uono na kushindwa kuongoza gari. Watu wengi wanaofanya safari maeneo ya mijini hawapaswi kutumia taa hizi kutokana na uwepo wa magari mengi na pia hakuna giza tororo.
Image result for high beam car lights gif

Taa za nyuma (Tail lights)
Taa hizi hutoa mwanga mwekundu upande wa nyuma wa gari na zimeunganishwa katika mfumo ambao utaziwasha wakati wowote ambao taa za mbele zimewashwa. Hii husaidia sana wakati wa giza dereva wa nyuma yako kutambua kwamba mbele yake kuna gari na atambue umbali uliopo baina ya gari lake na gari la mbele yake.
Image result for Tail lights
Taa za kutembelea mchana
Taa hizi hazipo katika magari yote, zinapatikana zaidi katika magari ya kisasa yaliyotengenezwa miaka ya hivi karibuni.
Taa hizi hupatikana katika maeneo yote ya nyuma na mbele ya gari na huwasha pale gari linapowashwa, japokuwa kwenye baadhi ya magari unaweza ukazizima.
Zimetengenezwa kutoa ishara na kukuwezesha wewe kuonekana zaidi na dereva anayekuja nyuma yako, lakini wengine hizizima kwa vile huona hazina maana sana. Baadhi ya watu huziacha ziwake kwani hutumika kama urembo wa kuongeza mvuto kwenye gari.
Image result for Daytime running lights
Taa za ukungu (Fog lights)
Taa hizi hupatikana karibu na taa za mbele. Kwa kawaida huwa zina mwanga mdogo ili kuzuia mwanga wake usiakisi katika ukungu na kukurudia wewe (dereva). Zinatakiwa kutumika tu endapo kutakuwa na ukungu ili kutoa ishara kwa madereva na watumiaji wengine wa barabara. Lakini madereva wengine huamua pia kutumia taa za mbele zenye mwanga mdogo kukiwa na ukungu.
Image result for fog light
Taa za ishara (signal Lights/ indicators)
Hizi hutumika zaidi katika kutoa ishara kwa madereva na watumiaji wengine wa barabara. Zinapatikana nyuma, pembeni (sio magari yote) na mbele ya gari. Mara nyingi zinakuwa pembeni ya taa za mbele na taa za nyuma.
Taa hizi hutoa ishara kwa dereva mwingine kuwa unataka kuingia upande fulani. Ukiwasha taa za upande wa kushoto itamaanisha unataka kuingia upande wa kushoto, vivyo hivyo na upande wa kulia.
Image result for indicator car lights gif
Taa za breki (Break lights)
Taa za breki zipo nyuma ya gari lako pembeni ya taa za nyuma. Kazi kubwa ya taa hizi ni kutoa ishara kwa dereva mwingine kuwa unapunguza mwendo au unataka kusimama.
Kwa vile taa hizi huwaka tu endapo utakanyaga breki, hakuna wasiwasi kwamba utaziwasha sehemu ambayo haihitajiki. Ila unatakiwa kuhakikisha kwamba zinafanya kazi vizuri kuepusha ajali.
Image result for Brake lights GIF
Taa za kuashiria hatari (Hazard lights)
Taa hizi hupatikana nyumba na mbele ya gari. Zipo sehemu moja na taa za kutoa ishara tulizozijadili hapo juu lakini hutofautiana kwa matumizi.
Taa hizi zinapowashwa huwaka na kuzima na hutoa ishara kwa madereva wengine kwamba umekumbana na tatizo kwenye gari liko hivyo wawe makini, au huashiria kwamba kuna hatari mbele kidogo (jiwe barabarani, ajali).
Zinatakiwa kutumika tu kutoa tahadhari kwa madereva wengine kama kuna tatizo kwenye gari au barabarani. Lakini pia unaweza kuzitumia taa hizi kama gari lako limesimama sehemu ambayo itasababisha usumbufu kwa watu wengine, lakini hii isiwe tiketi ya wewe kusimama popote.
Image result for hazard lights GIF
Taa za ndani ya gari (Driving lamps)
Hizi hupatikana ndani ya gari lako na hutumika na dereva au abiria wakati wa kuingia ndani ya gari, kutafuta kitu ndani ya gari kama kuna giza, au kuangalia ramani inayomuelekeza aendako.
Taa hizi hazitakiwi kuwashwa kwa muda mrefu ili zisije zikamuathiri dereva.
Image result for lamps inside the car
Taa za maegesho (Parking lights)
Hizi katika gari hutumika wakati wa kuegesha gari ambapo dereva hahitaji mwanga mkali wakati akiegesha gari. Kama unaegesha gari lako sehemu ambayo mbele kuna watu, si ustaarabu kuwamulika na taa yenye mwanga mkali, badala yake unawasha taa hii na inakupa mwanga kidogo kuwezesha kuegesha gari.
car reg check
Baadhi ya watu huendesha magari yao taa hizi zikiwa zinawaka hata kama ni mchana, na kwenye baadhi ya magari zimetengenezwa kuwa kama urembo ambapo hutumika wakati wa mchana.
Taa zinazoashiria gari kurudi nyuma (Reverse lights)
Taa hizi zipo nyuma ya gari na huwaka kwa rangi ya kung’aa kama taa za mbele. Matumizi makubwa ya taa hizi ni wakati wa kurudisha gari nyuma.
Taa hizi huwaka pale tu gia ya kurudi nyuma (reverse gear) inapoingizwa na dereva.
Taa hizi huwaka kwa mwanga mweupe ili kumuwezesha dereva kuona nyuma kwa ufasaha wakati gari likirudi nyuma hasa wakati wa usiku ama panapokuwa na mwanga hafifu.
Image result for reverse lights
Taa ya namba za gari (license plate lights)
Unapowasha gari taa za mbele za gari lako ili uweze kuona njia, taa hizi pia huwaka. Lengo kubwa la taa hizi ni kuonyesha namba ya usajili wa gari lako wakati wote.
Baadhi ya watu wakifanya uhalifu hukimbia wakitaka wasijulikane, lakini taa hizi zikiwa zinawaka, itawezekana kurekodiwa kwa namba za usajili wa gari lako kwa hatua zaidi.
Image result for license plate lights
Ni muhimu kuhakikisha kuwa taa zote kwenye gari lako zinawaka sawa sawa. Kuna baadhi ya taa ambazo kama hazifanyi kazi utatozwa faini lakini nyingine hautotozwa.
Taa za ndani ya gari na taa za ukungu si kosa kisheria kutokuwa nazo lakini ni muhimu kwa ajili ya kukurahisishisha kazi yako ya udereva. Kwenye upande wa taa za ukungu, sio magari yote yanazo, kwani tumeeleza awali kwamba baadhi ya madereva hutumia taa za kawaida.
Taa nyingine zisipofanya kazi ni kosa kisheria. Hakikisha unafanyia usafi taa zako kila mara ili kutoa mwanga wa kutosha na pia kuzibadilisha mara tu zipatapo tatizo.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: FAHAMU AINA NA MATUMIZI YA TAA MBALIMBALI ZA KWENYE GARI
FAHAMU AINA NA MATUMIZI YA TAA MBALIMBALI ZA KWENYE GARI
https://3.bp.blogspot.com/-utkE9GK5Fr8/WZyJssCJP_I/AAAAAAAAd40/1oeS__AtnEkKi8qgsTGqxz6LKwKjXoarACLcBGAs/s1600/16-561x375.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-utkE9GK5Fr8/WZyJssCJP_I/AAAAAAAAd40/1oeS__AtnEkKi8qgsTGqxz6LKwKjXoarACLcBGAs/s72-c/16-561x375.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/08/fahamu-aina-na-matumizi-ya-taa.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/08/fahamu-aina-na-matumizi-ya-taa.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy