FAHAMU UNAVYOWEZA KUPIMA KIWANJA KWA KUTUMIA SIMU YA MKONONI

SHARE:

TAASISI ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Utafiti lisilo la kiserikali (GRADE) lililopo nchi ya Lima...

TAASISI ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Utafiti lisilo la kiserikali (GRADE) lililopo nchi ya Lima, Peru zimetengeneza program ya simu ya mkononi inayoitwa LOTIZER inayoweza kutumiwa na wamiliki ardhi katika maeneo mapya ya mijini ili kupanga viwanja kabla ya kuuza.
Teknolojia hiyo mpya ya kupanga makazi ilioneshwa kwa viongozi, wananchi na watendaji wa mkoa wa Dar es salaam katika semina iliyofanyika katika ukumbi wa ESRF.
Programu  hiyo iliyotengenezwa baada ya kufanywa kwa utafiti unaohusu “Upangaji wa Hiari wa Makazi katika Jamii” katika Mkoa wa Dar es Salaam, imefunzwa pia kwa madalali.
Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho ESRF, Profesa Fortunata Makene akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dr. Tausi Kida kwenye warsha ya uenezaji wa programu ya kupanga makazi kwa wamiliki ardhi, madalali, viongozi wa mitaa na wataalamu iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano ESRF jijini Dar es Salaam.
Mradi huo wenye lengo la kuimarisha michakato bora zaidi ya kupanga miji katika nchi zinazoendelea, hususani kwenye makazi yasiyo rasmi inaweza kupakuliwa kutoka kwenye tovuti  ya “www.grade.edu.pe/lotizer na kuwekwa kwenye simu ya mkononi.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho Profesa  Fortunata Makene ambaye ni mmoja wa watafiti  waliozungumza na wananchi wa maeneo ya holela ya jijini Dar es salaam kama Kivule, Tandika, Tandale na Keko maghurumbasi, Program hii inaweza kutumiwa na wamiliki ardhi katika maeneo mapya ya mijini ili kupanga viwanja kabla ya kuuza.
Profesa Makene alisema kwamba  walifanya utafiti kuelewa sababu za kijamii, kiuchumi na kitamaduni zinazosababisha ukaaji wa watu katika makazi yasiyo rasmi maeneo ya mijini.
Mtafiti kutoka ESRF, Jires Tunguhole akiitambulisha na kuelekeza jinsi ya kupakua LOTIZER programu ya simu bure kabisa ambayo ni teknolojia mpya ya kupanga makazi wakati wa warsha ya uenezaji wa programu ya kupanga makazi kwa wamiliki ardhi, madalali, viongozi wa mitaa na wataalamu iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano ESRF jijini Dar es Salaam.
Aidha katika utafiti huo pia waliibua changamoto zinazowakabili wakazi waishio katika makazi yasiyo rasmi, yaani makazi holela na kutafuta suluhisho la kiteknolojia ya kuwasaidia wanajamii, hususani wenye maeneo ya kuuza, kuweza kupangilia viwanja kabla ya kuuza.
Imeelezwa kuwa mara tu inapowekwa kwenye simu, program hiyo inaweza kutumika kutengeneza mpango wa viwanja wenye ukubwa tofauti kutokana na upendeleo wa mmiliki ardhi.
Katika mahojiano na baadhi ya wananchi na watendaji waliofika katika semina hiyo ya maelekezo, walisifia uwapo wa teknolojia na kusema itasaidia sana kupanga miji.
Mtafiti kutoka ESRF, Jires Tunguhole akitoa maelekezo ya namna ya kupakua LOTIZER kupitia simu za Android bure ambayo unaweza kutayarisha mpango wa makazi wa viwanja kwa muda wa dakika moja tu wakati wa warsha ya uenezaji wa programu ya kupanga makazi kwa wamiliki ardhi, madalali, viongozi wa mitaa na wataalamu iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano ESRF jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa mtaa wa Msigani kata ya Msigani Elibariki Mollel alisema kwamba program hiyo ndio suluhu ya mipango holela kwani inaonekana kuwa na manufaa makubwa.
Alisema kwamba mafunzo hayo yamewafungua macho na kuwaweka katika hali ya kutambua umuhimu wa mipango miji na mpangilio.
Alisema program hiyo itaondoa matata yaliyopo sasa katika kuwekeza kwenye ardhi.
Naye dalali wa viwanja Hassan Poronmo wa Mambwepande alisema kwamba mafunzo waliyopata kuhusiana na mipango miji na uwapo wa program utawasaidia kushawishi wenye ardhi umuhimu wa mipangilio kwa kutumia program hiyo.
Mtafiti Mwandamizi wa ESRF, Prof. Haidari Amani (kulia) akifafanua jambo juu ya umuhimu wa upangaji makazi wakati wa warsha ya uenezaji wa programu ya kupanga makazi kwa wamiliki ardhi, madalali, viongozi wa mitaa na wataalamu iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano ESRF jijini Dar es Salaam.
Alisema wao awali walikuwa wanahaja ya fedha tu lakini kwa sasa baada ya mafunzo anaona kwamba watakuwa na ushawishi mkubwa zaidi kwa wenye maeneo wanayotaka kuyauza.
Mmiliki wa ardhi aliyejitambulisha kwa jina la Mwajuma Hemed wa Mivumoni maarufu kama Difenda alisema kwamba  mafunzo hayo yamemwezesha kutambua umuhimu wa mipango miji.
Aidha alisema kwamba programu iliyooneshwa inahakikisha usalama wa maisha ya wananchi kutokana na kuwapo kwa mpangilio murua.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi na Mtafiti Mshiriki wa ESRF, Yvonne Matinyi (kulia) akizungumza kuhusu mtrandao wa www.grade.edu.pe/lotizer ambapo mbali na kupakua program hiyo kuna video na miongozo ambayo itasaidia kujenga makazi mazuri katika maeneo tunayoishi wakati wa warsha ya uenezaji wa programu ya kupanga makazi kwa wamiliki ardhi, madalali, viongozi wa mitaa na wataalamu iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Awali  Prof. Fortunata Songora Makene, Mkuu wa Kitengo the Utafiti na Machapisho akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya Dk Tausi Kida – Mkurugenzi Mtendaji, Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) aliwashukuru washiriki wa semina hiyo na kusema kuwa utafiti walioufanya uliweza kutoa mchango katika juhudi za serikali kuweka mipango miji salama.
“Kwa hiyo utafiti huu ni muhimu katika kuchangia mipango ya serikali na pia kutoa ushauri wa kisera unaohusiana na upangaji wa makazi bora kwa maendeleo ya Tanzania.” alisema.
Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho Profesa Fortunata Makene akisisitiza jambo wakati wa warsha ya uenezaji wa programu ya kupanga makazi kwa wamiliki ardhi, madalali, viongozi wa mitaa na wataalamu iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano ESRF jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini washiriki wa warsha ya uenezaji wa programu ya kupanga makazi ambao ni wamiliki ardhi, madalali, viongozi wa mitaa na wataalamu wakichangia maoni na kubadilishana uzoefu katika warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF.
Pichani juu na chini ni sehemu ya washiriki wa warsha ya uenezaji wa programu ya kupanga makazi ambao ni wamiliki ardhi, madalali, viongozi wa mitaa na wataalamu iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano ESRF jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi walioshiriki kwenye warsha hiyo.
Picha ya pamoja ya washiriki wa warsha ya uenezaji wa programu ya kupanga makazi kwa wamiliki ardhi, madalali, viongozi wa mitaa na wataalamu iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano ESRF jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa ESRF, Profesa Fortunata Makene akielezea kuhusu kijarida cha mwongozo wa mipango miji kinachopatikana bure katika tovuti ya www.grade.edu.pe/lotizer wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Kulia ni Mtafiti Mwandamizi wa ESRF, Prof. Haidari na kushoto ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi na Mtafiti Mshiriki wa ESRF, Yvonne Matinyi.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: FAHAMU UNAVYOWEZA KUPIMA KIWANJA KWA KUTUMIA SIMU YA MKONONI
FAHAMU UNAVYOWEZA KUPIMA KIWANJA KWA KUTUMIA SIMU YA MKONONI
https://1.bp.blogspot.com/-M1bmMIm5dMY/WaANfaO0UGI/AAAAAAAAd9c/EIGFFR0GdIAG_4G-V5DcdbDsRNZuxCePgCLcBGAs/s1600/xJA3A9541-750x375.jpg.pagespeed.ic.-_vWodo95d.webp
https://1.bp.blogspot.com/-M1bmMIm5dMY/WaANfaO0UGI/AAAAAAAAd9c/EIGFFR0GdIAG_4G-V5DcdbDsRNZuxCePgCLcBGAs/s72-c/xJA3A9541-750x375.jpg.pagespeed.ic.-_vWodo95d.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/08/fahamu-unavyoweza-kupima-kiwanja-kwa.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/08/fahamu-unavyoweza-kupima-kiwanja-kwa.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy