FAHAMU WAKATI SAHIHI WA KUMUACHISHA MTOTO KUNYONYA

Wiki iliyopita ilikuwa ni maadhimisho ya Wiki ya Kunyonyesha ambapo wanawake na watu wegine mbalimbali walikuwa wakishirikishana masuala mbalimbali yanayohusu kunyonyesha mtoto. Swali moja ambalo lilibaki akilini mwa wengi ni, muda gani mtoto anatakiwa kunyonyeshwa?
Baadhii ya wazazi walisema kuwa unatakiwa kumyonyesha mtoto kwa muda wote ambao atataka lakini wengine wakikisitiza kuwa ni lazima uwepo ukomo wa kumnyonyesha mtoto.
Wataalamu wa afya wanashauri kuwa, katika miezi sita ya mwanzo, mtoto apewa maziwa ya mama yake pekee kisha baada ya hapo, unaweza kunyonyesha na kumpa vyakula vingine kwa muda ambao utaamua. Wazazi wengi huwanyonyesha watoto wao kwa kipindi cha miaka miwili.
Kumnyonyesha mtoto ni jambo muhimu sana, kwa mzazi na mtoto. Kwa upande wa mtoto, maziwa ya mama humsaidia kumpa kinga ya mwili ili kuweza kupambana na magonjwa.
Lakini, kwa upande wa mama, kumnyonyesha mtoto kunajenga uhusiano wa kimwili na kihisia baina ya mama na mtoto wakati zoezi zima la unyonyeshaji likiendelea.
Kadiri unavyoendelea kumnyonyesha mwanao, ndivyo utofauti wa uhusiano baina yako na mwanao unavyozidi kuongezeka, nikimaanisha kuwa mnazidi kujiweka karibu. Hakuna muda muafaka uliowekwa ambapo unatakiwa kumuachisha ziwa mwanao, lakini inashauri isiwe chini ya miaka miwili.
Wakati mwanao ni mchanga, huna haja ya kusema nitamuachisha kunyonya wakati fulani, Hata hivyo, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), unaweza kumnyonyesha mwanao hadi miaka miwili na zaidi.
Katika umri wa miezi sita, mwili wa mtoto unaweza kuanza kula vyakula tofauti tofauti. Wakati huo anaweza kukaa, kuchukua vitu na kuvikimbiza mdomoni.
Unaweza ukaanza kumpa vyakula vilaini wakati ukiendelea taratibu na vile vigumu. Akifikisha umri wa miaka miwili, atakuwa na uwezo wa kula vyakula vya kawaida ambavyo huliwa na watu wengine katika jamii.
Kuwa makini na ushauri wa rafiki zako kuhusu suala la kuachisha kumnyonyesha mwanao. Kama huna uhakika na lini uache, muone mtaalamu wa afya ambapo yeye ataangalia afya ya mwanao na kukushauri nini cha kufanya.
Je! Wewe (mwanamke) huwa unamnyonyesha/utamnyonyesha mwanao kwa muda gani? Unaweza kutuandikia maoni yako hapo chini na wengine wakajifunza zaidi kutoka kwako.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post