GIGY MONEY, BARNABA WADAI SI WAPENZI

Gigy Money
BAADA ya Gigy Money na Barnaba  kupiga picha wakiwa wamepakatana na kuzua gumzo kwenye mitandao ya kijamii wakidaiwa kwamba ni wapenzi, Elias Barnaba ‘Barnaba’ na muuza sura Gift Stanford ‘Gigy Money’ wameibuka na kudai kuwa wao si wapenzi.

Awali kulikuwa na nyepesinyepesi zikidai kuwa hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa wawili hao kuonekana wakiwa wamepakatana katika maeneo mbalimbali, wakisema baada ya Barnaba kuachana na mkewe, aliamua kujiweka kwa mwanadada huyo asiyeishiwa matukio mjini.
Barnaba.
Za Motomoto News ilipowasiliana na Barnaba, alisema Gigy Money ni dada yake kama walivyo madada wengine na katika maisha yake haishi kwa skendo hivyo wanaosema hivyo siyo kweli.
Kwa upande wake Gigy, alisema Barnaba ni kaka yake na pia shemeji yake, kwani ni rafiki wa aliyekuwa mpenzi wake, Mo J na hiyo picha walipigwa wakiwa kwenye shoo hivyo hakuna suala la mapenzi kati yao.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post