HAMISA MOBETO ALIAMSHA DUDE LA DIAMOND

Mwanamitindo Hamisa alijifungua tarehe 08/05/2017 na kuanzia kipindi cha miezi ya katikati ya ujauzito wake fununu zilianza kusambaa kwa washabiki kupitia mitandao ya kijamii zikidai kwamba Diamond ndio mzazi mwenzake huku yeye (Hamisa) akisema kwamba hana haja ya kumuweka wazi mpenzi wake wa sasa kwakuwa kufanya hivyo ilishamgharimu mara ya kwanza na kukana kuwa mhusika wa mimba yake yupo lakini si mwanamuziki Diamond.
Hamisa Mobeto ameliamsha dude ambalo bila shaka linaweza kuzua maswali mengi kwa wafuatiliaji wa tasnia ya sanaa nchini baada ya kujifungua hivi karibuni na kumuita mtoto wake jina linalofanana na Staa wa Bongofleva, Diamond Platnumz.
Kana kwamba alitaka kuzichochea au kuthibitishia mashabiki waliokuwa wakivumisha tetesi kwamba mhusika wa mimba aliyokuwa nayo ni Diamond Platumz, Hamisa ameamua kumuita mtoto wake huyo Abdul Naseeb, sawa na jina halisi la mwanamuziki kiongozi wa kundi la WCB.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post