HII NDIO ITAKUWA KAZI MPYA YA MZEE MAJUTO BAADA YA KUSTAAFU UIGIZAJI

Ingekuwa ni kwenye soka, tungesema kwamba ameamua kutundika daluga.
Alhaji Amri Athumani maarufu kwa jina lake la sanaa, Mzee Majuto amesema kwamba, ameamua kustafuu kufanya kazi za sanaa baada ya kufanya kazi ya uigizaji na uchekeshaji kwa miaka 30.
Mzee Majuto anayefahamika kwa uwezo wake mkubwa wa kukuvunja mbavu kutokana na mtindo wake wa kuigiza, alisema ameamua kustaafu na kwamba muda wake uliobakia wa kuishi hapa duniani atakuwa akimtumikia Mungu.
“Nimestaafu shughuli za sanaa, na sasa narudi kijijini kwangu ambapo nitakuwa nikimtumikia Mungu anisamehe dhambi zangu nilizozifanya.”
“Kuna mammbo mengi ambayo sisi kama wasanii huwa tunafanya ambapo baadhi ni mazuri, lakini mengine hayampendezi Mungu, ndio sababu tunahitaji kumuomba Mungu,” alisema Mzee Majuto.
Mzee Majuto alisema kwamba kwa sasa atakachoweza kufanya ni matangazo ya biashara tu na baada ya hapo atarejea kijijini kwake mkoani Tanga.
“Nina vifaa vyangu hapa, lakini nimeamua kuwaachia wanangu hii kazi ambao sasa wanawaweza kuanzia pale mimi nilipoishia,” alisema Majuto.
Majuto ambaye sasa ana umri wa miaka 69 amewahi kulitumikia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) pamoja na Jeshi la Zimamoto kwa miaka 20.
Majuto alianza shughuli za sanaa katika miaka ya 1980 wakati akifanya kazi na Mamlaka ya Bandari ya Tanga.
Mafanikio yake katika sanaa yalianza mwaka 1983 ambapo amewahi kufanyakazi na marehemu Kapteni John Komba wakiwa katika kundi la Tanzania One Theater (TOT).
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post