HII NDIYO BOMOABOMOA MPYA YA KUTISHA ITAKAYOLIKUMBA JIJI LA DAR ES SALAAM

Wakati vilio vya kubomolewa nyumba za makazi na biashara vikiendelea kuwatoka wakazi wa Kimara na Mbezi jijini Dar es Salaa, serikali imetangaza bomobomoa nyingine kubwa zaidi kuliko hiyo ya sasa.
Katika bomoabomoa hiyo mpya, serikali inatarajia kuvunja nyumba zaidi ya 17,000 zilizojengwa katika hifadhi ya Mto Msimbazi wilayani Ilala kuanzia vilima vya Pugu hadi Daraja la Selander.
Ofisa Mipango Miji wa Wizara ya Ardhi, Dk. Charles Mkalawa aliyembatana na Mwanasheria Mwandamizi wa wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Heche Suguti walisema kwamba zaidi ya nyumba 17,000 zilizojengwa kinyume na sheria katika Bonde la Msimbazi zitabomolewa.
Aidha, wameeleza kuwa, operesheni hiyo itawahusu pia wale wote waliojenga vibanda katika Bonde la Mkwajuni eneo la Magomeni wilayani Kinondoni na kuwataka wote walio katika maeneo hayo kujiandaa kuondoka kupisha shughuli hiyo.
Serikali imesema kuwa mwaka jana iliwataka wakazi hao kuondoka na walipokwenda mahakamani walishindwa lakini hawakuondoka huku wengine wakiendelea kujenga.
Ilielezwa kuwa, zuio la kujenga au kuishi katika eneo hilo liliwekwa mwaka 1945 lakini ilipofika miaka ya 1990, wakazi wengi wa Dar walivamia maeneo hayo na kuanza kujenga kinyume na sheria.
“Mfano hawa wenye vibanda ambavyo vinachomoza kila kukicha katika Bonde la Mkwajuni, tulishawapiga marufuku na hapa palikuwa peupe lakini wamerudi.Sasa nawaambia wajiandae kuondoka hapa, operesheni hii itawahusu,” amesema Heche
“Alipoulizwa bomoabomoa inaanza lini, Heche hakutaka kusema zaidi ya kusisitiza wananchi wajiandae kuondoka ili kupisha operesheni hiyo.”
Viongozi hao wamesema kuwa hakuna mwananchi atakayelipwa fidia katika bomoabomoa hiyo kwa sababu ni wavamizi. Dk. Mkalawa alisema mtu aliyevamia eneo huwa hapewi hata taarifa, unakwenda unamtoa kwa nguvu, lakini kwa sababu serikali hii ni ya huruma imewapa taarifa ili wajiandae kuondoka.
Mwanasheria wa NEMC alisema kuwa operesheni hiyo haitaishia Dar es Salaam peke yake na kwamba wakazi wa mikoani wajiandae kwani wote waliojenga kando kando ya mito, maziwa au vyanzo vya maji watabomolewa kwani nao ni wavamizi.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post