HISTORIA YA DENI LILILOSABABISHA NDEGE YA SERIKALI KUZUILIWA CANADA

Ndege mpya ya serikali aina ya Bombardier Q 400-Dash 8 iliyonunuliwa nchini Canada imezuiwa kuondoka nchini humo kutokana na Serikali kudaiwa fidia.
Ndege hiyo ilitakiwa iwasili nchini mwezi Julai, lakini hadi sasa hakuna taarifa kuhusu lini ndege hiyo itakuja nchini.
Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho alisema ndege hiyo inashikiliwa na kampuni ya Stirling Civil Engineering Ltd inayoidai Serikali dola 38.7milioni sawa na Sh87bilioni baada ya serikali kuvunja mkataba wa kampuni hiyo ya Canada iliyokuwa ikijenga barabara ya Tegeta WazoBagamoyo.
Baada ya mkataba kuvunjwa, Stirling ilifungua kesi Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi, ikidai kukiukwa kwa mkataba na ilipofika
Juni 2010, mahakama hiyo iliipa ushindi kwa kampuni hiyo, ikiitaka Serikali ilipe fidia ya dola 25 milioni za Kimarekani lakini hilo halikufanyika kama mahakama ilivyoamua.
Kufuatia hukumu hiyo, Tanzania ikakata Rufaa, tarehe 10 Juni 2010 hukumu ya rufaa ikasomwa ambapo kampuni hiyo ya ujenzi ya Canada ilishinda kwa mara nyingine.
Serikali iliamuriwa kuilipa kampuni hiyo fedha hizo vinginevyo kila mwaka mmoja utakaohesabiwa italipa na riba ya asilimia 8.
Kufikia Juni, 2017, deni hilo lilikuwa limeongezeka hadi dola za marekani 38.7 milioni sawa na Tsh 87 bilioni kutokana na ucheleweshaji wa malipo.
Lissu alisema, Juni 30 mwaka huu mahakama hiyo iliipa kampuni ya Stirling kibali cha kukamata mali zote za Tanzania zitakazokuwa katika nchi za Ufaransa, Uholanzi, Uingereza, Ubelgiji, Uganda na Canada.
Aidha, Lissu alisema licha ya Waziri Mahiga kwenda nchini Canada kukutana na kampuni hiyo kwa ajili ya mazungumzo ili ndege hiyo iweze kuja nchini, alidai kwamba alikataa hadi walipwe kwanza dola za Marekani 12.5 milioni sawa na Tsh 28 bilioni.
Wakati ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali ikizungumza na waandishi wa habari alisema ni kweli kuna mgogoro katika ununuzi wa ndege hiyo lakini hakuweka wazi ni mgogoro wa nini na kwamba ndege hiyo itakuja lini.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post