HIVI NDIO VITUKO VITANO VYA RAIS MUGABE WA ZIMBABWE

Mbali na hotuba zake za kupinga nchi za Magharibi kuingilia au kutaka kushawishi tawala za nchi za Afrika na uamuzi wake wa kuwapokonya ardhi wazungu nchini Zimbabwe mwanzoni mwa miaka ya 2000, Robert Mugabe anasifika kwa kuwa mchekeshaji mzuri kiasi cha kusemwa kwamba anaweza kushindana na wachekeshaji maarufu zaidi duniani.
Rais huyu wa Zimbabwe amekuwa kiongozi mkuu wa nchi hiyo kwa miaka 36 sasa. Pia, huwa anatoa kauli tata sana kiasi cha kufanya mwanasiasa mtukutu wa nchini Afrika Kusini, Julius Malema aonekane malaika mwema kabisa.

Kumchumbia Rais Obama

Miongoni mwa mambo yanayofurahisha wengi sana ni tukio la harusi. Lakini Rais Mugabe alipotangaza kwamba ana mpango wa kumchumbia na kumvalisha pete ya uchumba Rais Obama, wengi walishangazwa. Akiongea katika kituo cha utangazaji cha taifa, Rais Mugabe alisema, “Nimeshaamua – kwakuwa Rais Obama anaunga mkono ndoa za jinsia moja, ahamasisha watu wenye uhusiano wa jinsia moja na anazungumzia kwa furaha – kwahiyo itabidi nisafiri kwenda Washington DC, nipige goti na kumvalisha pete ya uchumba kwenye kidole chake.” Nani angejuwa kwamba Obama angepata bahati kubwa kiasi hiki?
Hata hivyo, Rais Mugabe akabadili gia ghafla na kuanza kuishambulia Mahakama ya Juu Zaidi ya Marekani kwa kutoa uamuzi wa kuidhinisha ndoa za jinsia moja katika majimbo yote 50 nchini humo.

Kufa na kufufuka mara nyingi

“Nimeshakufa mara nyingi sana – kwenye hilo ndio nimemzidi hadi Yesu. Yesu alikufa mara moja na akafufuka mara moja tu,” hiyo ni kauli maarufu sana aliyowahi kuisema Rais Mugabe. Kwa mtu anayedaiwa kufariki kila unapofika mwezi Januari, nukuu hii inatoa muhtasari wa kila kitu. Kwahiyo, ni nini siri ya kufufuka hukwa kwa Mugabe? “Kuna baadhi ya mambo inabidi mtu ujifanyie. Usinywe pombe kabisa, usivute sigara, lazima ufanye mazoezi na ule mboga za majani na matunda kwa wingi.” Hiyo ndio siri kubwa kama unataka kuwa unakufa na kufufuka kila mwezi Januari. Ikiwa baadhi ya wanafunzi nchini Zimbabwe wakitaka siku ya Februari 21 (Siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa Rais huyo kuwa sikukuu ya kitaifa), labda anastahili Pasaka yake kila anapofufuka ili amzidi Yesu kwenye hili pia.

Kuhusu raia wa Zimbabwe wanaoishi Uingereza

“Uingereza kuna baridi sana, ni nchi isiyofaa kuishi kwakuwa nyumba zake ni ndogo sana.” Hapa Rais Mugabe alikuwa akizungumzia raia wa nchi hiyo waliokuwa wakiishi uhamishoni Uingereza ambao alisema watu hao bila shaka walikuwa wanatumia jina lake kupatiwa hifadhi na kusema “Kama ukisema ‘Mugabe’, lazima watakwambia ‘karibu, karibu’…. lakini waangalie sasa, wameanza kulalamika kwamba watu wamezidi, wanasababisha wasiwasi kwa Waingereza, ngoja tuwarudishe kwao.” Aliwaomba warudi nyumbani waondoke kwenye nchi yenye baridi kali na vijumba vidogo akiwaahidi kazi mpya na uchumi bora.

Alivyomropokea Askofu Desmond Tutu kwenye kadamnasi

Baada ya Askofu Desmond Tutu wa Afrika Kusini kusema kwamba Rais Mugabe ni mfano mzuri sana wa madikteta wa Afrika kwamba ni kinyago kichotengenezwa na baadaye kumtisha aliyekitengeneza, Rais Mugabe hakuweza kumkalia kimya. Aliamua kuikuza mada hiyo kwa kusema mbele ya kadamnasi, “Kale (Desmond Tutu) ni kaaskofu kadogo sana kenye hasira, kaovu na kenye chuki binafsi.” Kauli hii aliitoa mwaka 2004 lakini mwaka 2013 Mugabe alimchokonoa tena Askofu huyu wa Kanisa la Anglikana, safari hii kwa msimamo wake wa kuunga mkono uhusiano wa jinsia moja.
“…. eti tuna mwanaume anayeheshimika, tena ana cheo cha Askofu. Tutu anatakiwa kujiuzulu kwa sababu anaunga mkono wanaofanya mapenzi ya jinsia moja, jambo ambalo ni ovu kabisa. Sisi hawatutaki watu wa aina hii.”
Labda vita yao hii ya maneno ilisababishwa na kila mmoja kumchukia mwenzie kwa sababu Askofu naye alibwatuka mara moja kwa kusema, “Namsikitia Mugabe kwa kila namna ambayo mtu anaweza kufikiria kwa sababu alikuwa kiongozi mzuri sana miaka ya nyuma.”

Alipozungumzia kiwango kikubwa cha rushwa nchini Naijeria

“Inamana tumekuwa kama Naijeria kwamba unatakiwa kuingiza mkono mfuko ili upate kila unachohitaji?”, ndio lilikuwa swali lake. Kauli hii ilitolewa na Rais Mugabe alipokuwa akizungumza kwenye chakula cha mchana katika sherehe ya kutimiza miaka 90 na kuendelea, “Ukipanda ndege nchini Naijeria basi utaona wahudumu wa ndege wanajizungusha tu bila kuruhusu ndege ipae mpaka wapewe rushwa.”
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post