HIZI NI SABABU TANO ZA KUKUFANYA UMUAMINI MPENZI WAKO

Mpenzi wako anapokuamini huwa inasaidia sana kufanya uhusiano wenu uwe mzuri zaidi na kutawaliwa na upendo wa hali ya juu. Ni moja ya mambo yanayofanya uhusiano udumu kwa muda mrefu sana. Kuaminiana ndio msingi mkubwa wa mahusiano yote ya binadamu, kuanzia uhusiano wa muda mfupi tu kutokana na kujikuta kwenye mazingira ya aina moja, urafiki usiohusisha mapenzi mpaka kwenye uhusiano wa kimapenzi. Huongoza na kusaidia kutabiri uelekeo wa uhusiano tulionao kwa watu wengine.
Uwezo wa watu kuamini au kuaminika unatofautiana sana kwakuwa wapo wanaoweza kuamini kirahisi kuliko watu wengine na pia wanaaminika zaidi na wana uwezo mkubwa wa kujua mtu mwenye sifa kama hizo.
Kukusaidia kugundua iwapo unastahili kumuamini mpenzi wako kwa kiasi kikubwa zaidi ya unavyomuamini sasa, hizi ni ishara au vigezo vitano ambavyo inabidi uviangalie kwake. Iwapo anavyo – basi jua umeokota embe dodo chini ya mnazi na uithamini bahati hiyo na kuilinda usiipoteze:

Mpenzi wako ni muwazi kwako

Mshawahi kuambiana mawazo au hisia zenu za ndani kabisa bila kuogopa kwamba mwenzako atakuumiza? Hii ni ishara ya kweli kabisa kwamba upo na mtu ambaye anaaminika. Watu wenye vitu vya kuficha mara nyingi hawawezi kuweka hisia zao wazi bila kuogopa. Wanatoa visingizio na vikwazo vingi ili usiweze kujua ukweli waliouficha na ni rahisi kuwakamata wanaposema mambo ya uongo ambayo yanapishana na waliyowahi kuyasema mwanzo. Ikiwa mpenzi wako anakwambia mambo yake na hisia zake na wewe kuweza kupatwa na hisia zake kiundani, basi ujue upo kwenye uhusiano na mtu anayekupenda na kukuamini sana.

Mpenzi wako anakutambulisha kwa watu wa karibu na muhimu kwake

Watu wenye uhusiano zaidi ya mmoja huwa hawawezi kuweka wazi uhusiano wao kama kwenye mitandao ya kijamii au kujiweka wazi ili wajulikane na watu wengine. Mara nyingi wakipigiwa simu wakiwa na wapenzi wao utaona wanatoka kwenda kuongelea pembeni ili wasisikike wanachoongea. Wanaweka maneno ya siri (password) kwenye vitu vyao vingi. Kama unaona mpenzi wako anakuzungumzia na kukumwagia sifa waziwazi na kusifu uhusiano wenu, jua wazi kwamba upo na mtu ambaye amekuweka kipaumbele kwenye maisha yake. Kama mpenzi wako anakutambulisha kwa familia yake, marafiki na watu wengine wanaomzunguka, jua kwamba hana cha kukuficha kabisa.

Mpenzi wako anajali uhusiano wenu

Kama mpenzi wako anapenda kuwa na wewe na anaonesha kwamba ninyi ni kitu kimoja basi unastahili kumuweka karibu sana hasa ikiwa anakuthamini zaidi kadri ya muda unavyoendelea kwenda. Kumfanya mtu akuamini haihusiani na kumthibitishia chochote. Kama imani inaonekana kwa yeye kukushirikisha kwenye shughuli za familia na marafiki zake, basi ukubali kwamba hisia zake ni za kweli na uziheshimu. Kukujali ni njia mojawapo ya kukwambia, “Nipo na wewe. Siendi popote, niamini kwa hilo. Ikiwa mshapitia nyakati ngumu na majaribu mengi na bado unamuona amebaki na wewe, hiyo ni dalili uhusiano una uelekeo mzuri sana.

Mpenzi wako yupo kila unapomuhitaji

Ni rahisi kujua kama mtu yupo na wewe kwa muda mfupi tu au mtakuwa pamoja kwenye milima na mabonde. Hili linathibitika mnapokumbana na vikwazo na majaribu, hapo ndipo hasa maisha ya kujuana yanapoanza. Dunia inapowatupia vikwazo vyote ilivyonavyo na kuongeza vingine zaidi. Kama mpenzi wako ataendelea kubaki na wewe mpaka dhoruba hizo zipate, basi ni wa kumwamini. Watu wengi ambao hawana haja ya kuwa na wewe kwa muda mrefu hawawezi kukubali kuwa na wewe kwenye vipindi vya shida. Unapojitolea kujijali na kujithamini wewe mwenyewe, watu wanaokuzunguka watakuchukulia hivyo hivyo. Uhusiano wa hauwi mzuri tangu mwazo mnapokutana. Unajengwa kupitia kumwamini na kuaminiwa na mpenzi wako mnavyozidi kuwa pamoja kwenye mapenzi yenu.

Mpenzi wako anakufanya ujione salama zaidi

Ukiwa na mtu anayekufanyia ujione upo mahala salama zaidi unapokuwa karibu naye, ujue una mtu anayestahili kuaminiwa. Mpenzi anayekusaidia na kukufanya usiwe na msongo wa mawazo ya kimaisha kwa kupambana na changamoto zako ni mtu ambaye bila shaka unatakiwa umwamini. Anahitaji na kukuombea mafanikio makubwa kabisa maishani mwako. Amekuona ukiwa katika hali mbaya kabisa. Amekuona ukiwa kwenye majanga makubwa lakini bado amekuwa na wewe kwa zaidi ya hali yako. Huu ndio muda ambao bila shaka inabidi urudishe hisia kama anazokuonesha. Kama anaonesha kukuamini basi ujue na yeye anastahili kuaminiwa. Kama mpenzi wako anafanya anayoahidi na kufanya mambo bila kutegemea malipo kutoka kwako, na bado anaendelea kuwa nawe na kukupenda kwa dhati, huyu ni mtu unayestahili kumwamini.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post