IDRIS NA WEMA SEPETU WAPASHA KIPORO MOTO

Kuna msemo wa kiswahili unaosema kuwa, wagombanao ndio wapatanao. Huenda msemo huo ukaweza kutumika kuelezea kinachoendelea kati ya mastaa wawili wa bongo, Idris Sultan na Wema Sepetu.
Baada ya kuachana kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, wawili hao wameanza kuwa karibu tena huku wakisifiana kupitia kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii hali ambayo haikuwepo katika kipindi cha nyuma.
Saa chache zikiwa zimesalia kabla ya Idris hajazindua brand yake mpya hapo kesho Agosti 20, 2017 Wema Sepetu katika ukurasa wake wa Instagram amechapisha picha ya Idris huku akimmwagia  sifa na kusema kuwa hawezi kuacha kumsifia kwani amekuwa akifanya kwa ubora vitu vyake.
“Nikisema sitojivunia ntakuwa ni muongo na mnafki… Proud of you sana… Cant wait for these babies to launch… Im sure zitakuwa Killer… Cause one thing I know is that “Classy” defines you alot better than anything…๐Ÿ˜Š #SultanXForemen… Goodmorning World..” aliandika Wema Sepetu.
Saa chache baadae, Idris alichapisha picha akijibu mapigo ambapo alianza kwa kushangazwa kwani amedai hakuwa na mawasiliano na Wema hivyo kum-post kumemshangaza, lakini akasema watu wasishtuke kwa kuwa Wema ni mke wake na mke huwa haachwi hata aolewe na mwanaume mwingine.
“MOOD: Unakuta kakuposti tu wakati mmekulana block hadi kwenye email ๐Ÿ˜‚… Dahhh ๐Ÿ™ˆ we mwanamke utakuja uniue ๐Ÿ˜….. Thank you mke ๐Ÿ˜‰ … Msishtuke, kwanzia lini mke anaachwa hata aolewe๐Ÿ˜‚. Mungu Ibariki hii launch jamani #sultanXforemen;.”
Wawili hao walikuwa ni wapenzi ambapo walishika kasi kwenye mitandao ya kijamii wakiwa wanazungumziwa kwa mambo tofauti tofauti, lakini baadae waliachana.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post