IDRIS SULTAN: UCHEKESHAJI UMENIPA MAISHA MAZURI

Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania Idris Sultan amefunguka faida alizozipata baada ya kuingia kwenye tasnia ya uchekeshaji.
Akizungumza na Zote kali, mshindi huyo ya Big Brother Africa 2014 amesema uchekeshaji umempa vitu vingi sana katika maisha yake ambavyo hakuwahi kufikiria hata siku moja kama anaweza kuvipata.
“Unajua comedy haikuwa kama kazi maalum kwangu ilikuwa kama njia tu yakuweza kupitia  kwasababu plan yangu kubwa ilikuwa kwenda Hollywood na kuna njia nyingi sana za kufikia huko,” amesema.
“Ila mimi nilichagua uchekeshaji, ingawa nilijitafuta kwenye njia nyingi ikiwemo pia host so comedy imenifanyia vitu vingi sana.
Nimeweka my brand kupitia comedy, nimeweza kuwa na kipindi changu cha Sio Habari” kupitia hiyo hiyo comedy na ni mtu pekee ambaye sio mwanamuziki, sio mwanamke  na bado nipo kwenye idadi ya watu maarufu mwenye followers wengi Instagram,” ameongeza Idris.
Alhamis hii Idris atazindua viatu vyake, Sultan X Foremen.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post