IGP SIRRO AELEZA SABABU YA MAUAJI YA KIBITI

Hatimaye Jeshi la Polisi limeeleza kiini cha mauaji yaliyokuwa yanafanywa katika Wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji mkoani Pwani ambapo watu 40 wakiwamo askari polisi 15 wameripotiwa kuuawa kwa kupigwa risasi katika Wilaya hizo tangu mauaji hayo yalipoanza mwaka 2015.
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro katika mahojiano na kituo cha ‘Radio One’ alisema uchunguzi waliofanya umebaini kuwa wauaji hao walikuwa wanalipa kisasi kwa kile alichodai kuwa ni hisia za kutotendewa haki na baadhi ya watendaji wa Serikali na maofisa wa jeshi hilo.
IGP Sirro alisema kuwa imechukua muda mrefu kwa jeshi hilo kukabiliana na wahusika wa mauaji hayo kutokana na wauaji kujipenyeza ndani ya jamii ya Wilaya hizo kwa karibu muongo mmoja, hivyo kuwa sehemu ya wakazi wa maeneo husika.
“Waliingia kwenye maeneo hayo (Kibiti, Mkuranga na Rufiji) miaka nane kabla ya kuanza mauaji,” alisema IGP Sirro na kuongeza, “walijipenyeza kwa njia mbalimbali, unadhani wanaendesha mafunzo ya kidini kumbe kinachofanyika ni mambo tofauti kabisa.”
“Waliwapotosha watu kwamba ‘elimu hii mnayopewa haina maana.’ Wakawafundisha Karate, Judo na namna ya kutumia silaha,” alisema.
Alisema kuwa operesheni iliyofanywa kwenye maeneo husika imefanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa kadhaa wa mauaji hayo lakini baadhi yao wamekimbilia maeneo mengine ya nchi.
Amewataka viongozi wote wa Kamati za Ulinzi na Usalama kuanzia ngazi ya Mtaa wahakikishe wanatoa taarifa za kuwafichua wahusika wa matukio hayo katika maeneo yao, akibainisha kuwa mara nyingi wamekuwa wakinunua maeneo makubwa na kuyatumia kwa mafunzo yao kwa siri.
Katika mahojiano hayo, IGP Sirro alisema kuwa uchunguzi wao umebaini kikundi hicho hakina sifa za kigaidi ispipokuwa ni “cha kijambazi tu.”
HT @ Nipashe
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post