IMETHIBITIKA: MAGANDA YA MAYAI YANATAKIWA KULIWA PIA

Uchunguzi uliofanyika hivi karibuni nchini Marekani unasema kuwa sasa ni wakati wa kuacha kutupa maganda ya mayai kwakuwa yana madini ambayo yana faida kwa binadamu. Badala ya kuyatupa maganda haya, kwanini usiongeze faida zaidi ya ile ya kula yai lenyewe?
Wataalamu wamegundua kwamba maganda ya mayai yana kiwango kikubwa sana cha madini aina ya Kalshiamu kwa sababu yanaundwa kwa madini ya ‘Calcium Carbonate’ kwa asilimia 95.
Ganda la yai moja linakadiriwa kuwa gramu mbili za madini ya Kalshiamu ambacho ni kati ya mara mbili hadi nne ya kiwango cha madini haya kinachohitajika na mwili wa binadamu kwa kila siku moja.
Lakini usikimbilie kuyabugia maganda ya mayai moja kwa moja baada ya kuyapasua na kula kilichomo ndani.
Kwanza inabidi uchemshe maganda haya ili kuua vijidudu vyovyote vinavyoweza kuwa vimeng’ang’ania. Kisha uyaoke (bake) kwenye nyuzijoto za sentigredi 93 kwa muda wa kati ya dakika kumi hadi kumi na tano.
Baada ya kuoka yasage ili yatengeneze unga. Unga uliotokana na kusaga maganda ya mayai unasemwa kuwa chanzo kizuri sana cha madini ya Kalshiamu mwilini. Pia unga huo umethibitishwa kupunguza maumivu na kupungua kwa mifupa kwa wanawake kutokana na ugonjwa wa Senile Osteoporosis, ugonjwa wa mifupa unaowapata wanawake kutokana na uzee au upungufu wa madini ya Kalshiamu mwilini.
Pia, unaweza kuongeza unga huu wakati unaandaa vyakula mbalimbali kama pizza, mkate, tambi na vinginevyo.
Lakini kuwa makini kwa sababu madini haya yanapozidi sana au kupungua sana mwilini yaweza kukuletea madhara kiafya. Mtu mzima mwenye afya bora anahitaji gramu moja tu ya madini ya Kalshiamu kwa siku.
Tazama video hii kujua jinsi ya kuandaa unga huo:JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post