JINSI JIKO LA MKAA LILIVYOSABABISHA HASARA YA BILIONI 14 SOKO LA SIDO, MBEYA

“Baada ya kufanya uchunguzi wa kina, Kamati yangu imejiridhisha kuwa chanzo cha moto ulioteketeza soko ni jikola mkaa ambalo liliachwa ndani ya mojawapo ya vibanda vya mamalishe ambapo Kamati ilikuta mabaki ya jiko hilo, majivu ya mkaa wa kupikia ambayo ni tofauti na ya mbao zilizoungua,” alisema Hassan Mkwawa, Mwenyekiti wa Kamati ya kuchunguza chanzo cha moto ulioteketeza soko la wafanyabiashara wadogo jijini Mbeya linalojulikana zaidi kwa jina la Sido alipokuwa akiwasilisha ripoti ya kamati yake kwa Mkuu wa Mkoa huo, Amos Makalla..
Kamati hii imebaini kuwa chanzo cha moto ulioteketeza soko la Sido jijini Mbeya imekamilisha kazi hiyo na kubaini kuwa chanzo cha moto huo ni jiko la mkaa lililoachwa likiwaka ndani ya kibanda kimojawapo cha mamalishe sokoni hapo ambapo pia imeainisha kuwa moto huo umesababisha hasara ya shilingi bilioni 14 kutokana na kuteketea kwa kuungua kwa moto mali za wafanyabiashara wa eneo hilo, majengo na miundombinu mbalimbali ya soko hilo.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya kuchunguza chanzo cha moto huo (Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbeya), Hassan Mkwawa, alisema kuwa kamati imejiridhisha kuwa chanzo cha moto huo ni jiko la mkaa baada ya kukuta majivu ya mkaa wa kupikia ambayo ni tofauti na majivu ya mabaki ya vitu vilivyoteketea katika kibanda kimojawapo cha mamalishe na ambacho kinasadikiwa kuwa ndipo moto huo ulipoanzia.
Mkwawa alisema kuwa katika kibanda hicho kinachosadikiwa kuwa moto ulianzia, hakuna umeme na hivyo hakuna dhana wala hisia zozote zinazoweza kuthibitisha kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amesema kuwa msimamo wa Serikali ni kwamba wafanyabiashara hao wataendelea kubaki eneo hilo ili waendelee na shughuli zao lakini amewataka sasa wajenge vibanda vya kudumu na si vya mbao kama vya awali ambavyo vinasababisha hasara kubwa linapotokea tukio kama hili.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post