JOYCE KIRIA AELEZA BANGI ZILIVYOMKOMESHA

Joyce Kiria.
MTANGAZAJI maarufu Bongo, Joyce Kiria amefunguka jinsi alivyokomolewa na kitendo chake cha kuvuta bangi, akidhani kingempa ujasiri, lakini badala yake akajikuta akishindwa kabisa kufanya kitu alichokusudia.
Akizungumza na Za Motomoto News, Joyce alisema kwa mara ya kwanza alivuta bangi alipoanza utangazaji katika kituo kimoja cha redio kipindi hicho na alifanya hivyo ili apate ujasiri wa kutangaza kwani alikuwa hajui, lakini aliambulia kuona vitu viwiliviwili na kushindwa kabisa kutangaza.
“Nimewahi kuvuta bangi mara moja ili niweze kutangaza maana nilikuwa naogopa, lakini nilipofika studio nikawa naona mic mbilimbili, watu wawiliwawili mwisho nikarudi nyumbani ambako nilikaa siku mbili nzima ndiyo nikawa sawa, sijawahi kurudia tena na sina mpango maana nilikoma siku hiyo,” alisema Joyce.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post