KATI YA AMBER LULU NA YOUNG D NANI KAVUJISHA PICHA ZA UTUPU?

Baada ya kusambaa kwa picha yake chafu akiwa na Video Queen matata wa Bongo, Amber Lulu kwenye mitandao ya kijamii, hitmaker wa Ngoma ya Bongo Bahati Mbaya, David Genzi ‘Young D’, ameomba radhi kwa Watanzania kupitia ukurasa wake wa Instagram.
“Nasikitishwa kwa picha inayosambaa mitandaoni, imevuja bila ridhaa yangu, ni picha iliyokuwa imepigwa behind the scene, lengo hasa la photo shoot ni aina hii mpya ya mavazi ya aina ya ki”Scottish” kama sketi. Naomba radhi sana kwa hili! Na kwa mashabiki wote, inauma sana,” ameandika Young D.
Saa chache baada ya posti hiyo, Amber Lulu naye akajibu mashambulizi.
“Mimi kiukweli hakuna ninachofahamu hizo picha ni za siku nyingi kipindi cha Bongo Bahati Mbaya na hiyo picha hakuwepo kwenye hizo picha ambazo ndiyo zilistahili kutoka sasa Youngdaresalama, unasema mimi nimevujisha ili iweje, mimi sina picha hata moja wewe. Hiyo uliitoa wapi? Uliyoposti mara ya mwisho zinafanana zote za sketi au kwakuwa ndiyo Amber ameshazoeleka na vichupi kwa hiyo hata hiyo unaona ni mimi tu siyo hivyo jamani mimi sijui chochote uchunguzi ufanyike tujue usikute watu wana hasira za kufutwa (tattoo).
Naomba radhi kwa hili lililotokea sijui chochote,” ameandika Amber Lulu.
Young D na Amber Lulu waliwahi kudaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi, lakini baadaye wakamwagana na kubaki kuwa marafiki.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post