KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA MADOLA AMTEMBELEA RAIS MAGUFULI IKULU

SHARE:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Agosti, 2017 amekutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya M...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Agosti, 2017 amekutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Patricia Scotland ambaye amemueleza juu ya mipango na mikakati mbalimbali ambayo Jumuiya hiyo inaiweka kwa lengo la kuhakikisha nchi wanachama zinanufaika na kuwemo kwao ndani ya Jumuiya hiyo.
Mhe. Patricia Scotland ametaja baadhi ya mipango hiyo kuwa ni kuongeza fursa ya kufanya biashara miongoni mwa nchi wanachama kutoka asilimia 19 ya sasa hadi kufikia asilimia 30, kuwasaidia wanawake na vijana na kuwezesha upatikanaji wa ajira kwa vijana ambao idadi yao ni wastani wa asilimia 60 ya watu wote, kutunza mazingira na kutumia ipasavyo fursa ya ukanda wa bahari kwa wanachama wake.
“Mhe. Rais tunaona kuna kila sababu ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kujiimarisha, tunazo fursa nyingi za kutuwezesha kutoka hapa tulipo na kuwa na umoja ambao una manufaa makubwa kwa wanachama wake, tunataka hili kundi kubwa la vijana ambalo kwa hapa Tanzania nimeambiwa ni asilimia 65 ya idadi ya watu wote, lipate matumaini na kuzalisha zaidi” amesema Mhe. Patricia Scotland.
Mhe. Patricia Scotland amesema wakati uchumi wa dunia ukikua kwa wastani wa asilimia 2, Bara la Afrika na Asia ambako kuna wanachama wengi wa Jumuiya ya Madola uchumi wake unakuwa kwa asilimia kati ya 5 na 8 na kwamba hii inatoa fursa zaidi kwa wanachama wa Jumuiya hii kupiga hatua na ametaja maeneo ya kipaumbele yatakayochochea ukuaji wa uchumi kuwa ni miundombinu na nishati.
Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amempongeza Mhe. Patricia Scotland kwa jitihada hizo na amemhakikishia kuwa Serikali yake inaunga mkono na ipo tayari kushirikiana na nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kukuza biashara na uwekezaji.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amekutana na Rais wa Mashirika ya Kipapa kutoka Vatican Mhashamu Baba Askofu Protas Rugambwa ambapo pamoja na kufanya nae mazungumzo amemkabidhi zawadi ya sanamu ya Bikira Maria wa Fatima na Rozari takatifu kutoka Vatican kwa ajili ya kufanyia ibada.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
10 Agosti, 2017

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA MADOLA AMTEMBELEA RAIS MAGUFULI IKULU
KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA MADOLA AMTEMBELEA RAIS MAGUFULI IKULU
https://1.bp.blogspot.com/-FY__g8BQhlQ/WY1P1kRPx0I/AAAAAAAAdXU/GwZE6Zzrny8op7T9qAzi2PlQN27uBKmtACLcBGAs/s1600/xunnamed-62-750x375.jpg.pagespeed.ic.zkhtr9VtEJ.webp
https://1.bp.blogspot.com/-FY__g8BQhlQ/WY1P1kRPx0I/AAAAAAAAdXU/GwZE6Zzrny8op7T9qAzi2PlQN27uBKmtACLcBGAs/s72-c/xunnamed-62-750x375.jpg.pagespeed.ic.zkhtr9VtEJ.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/08/katibu-mkuu-wa-jumuiya-ya-madola.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/08/katibu-mkuu-wa-jumuiya-ya-madola.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy