KENYA: MWANAFUNZI ALIYEFANYA KAMPENI KWA BASKELI ASHINDA UCHAGUZI

Mgombea binafsi katika uchaguzi mkuu wa Kenya mwenye umri wa miaka 24 ameshinda kiti cha ubunge katika jimbo la Igembe Kusini katika Kaunti ya Meru baada ya kuwapita wapinzani wake.
John Mwiringi ambaye alikuwa akifanya kampeni kwa njia ya baskeli amepata kura 19,366 akimzidi mgombea wa Chama cha Jubilee, Joseph Mwereria mwenye kura 15,724.
“Tuliamua kumchagua. Alikuwa hana fedha kwa ajili ya kampeni lakini alikuwa na sera nzuri na ilani yake ni nzuri sana,” mkazi mmoja wa eneo hilo alisema.
Mwirigi ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Mount Kenya, na huenda akawa mbunge mwenye umri mdogo zaidi ndani ya bunge la Kenya. Kampeni zake zilifadhiliwa na wafuasi ambapo kipindi cha likizo amekuwa akifanya kazi kama dereva bodaboda.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post