KIBA AKINUKISHA: MASTAA, VIONGOZI WAJITOSA!


DAR ES SALAAM: Amekinukisha! Si kwa ubaya, la hasha. Kwa wema tu. Mkali wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ amekinukisha kwa kuvunja rekodi ya kuzungumzwa na kutazamwa zaidi kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, saa chache baada ya kuachia wimbo wake mpya wa Seduce Me, Risasi Mchanganyiko limekusanya ripoti ya kuthibitisha hilo.

Kiba aliuachia wimbo huo, Ijumaa iliyopita na kusababisha ‘vurugu’ kubwa mitandaoni. Ndani ya saa 22 tangu wimbo huo uachiwe na kuwekwa katika mtandao wa YouTube, ulitazamwa na watu wasiopungua milioni 1.

MITANDAO YACHAFUKA

Mara baada ya Kiba kuuachia wimbo huo, ndani ya saa chache mitandao karibu yote ‘ilichafuka’ kwa watu kuposti vionjo vya wimbo huo huku kila mmoja akionesha hisia zake kwa kuweka kipande cha wimbo kilichomgusa.

WALINGANISHWA, WAIBUKA KIDEDEA

Kutokana na jinsi ulivyotazamwa na watu wengi, mashabiki mbalimbali walianza kuulinganisha na wimbo wa msanii mwingine ambaye naye aliachia wake muda mchache tu baada ya mwimbaji huyo wa kibao cha Aje kuachia Seduce Me, lakini bahati mbaya akajikuta akiangukia pua kwani mashabiki hawakuutolea macho kama alivyotarajia.

“Kiba tafadhali next time usituue kiasi hiki. Hili ni zaidi ya balaa, wimbo mtamu hadi umepitiliza. Umeuficha kabisa ule wa yule msanii mwingine aliyejifanya kuachia wimbo sambamba na wewe,” aliandika mdau mmoja katika mtandao wa Instagram.

VIONGOZI WA SERIKALI WAJITOSA

Kuonesha kwamba muziki wa Kiba haujawahi kumuacha mtu salama, viongozi wa serikali nao hawakuwa nyuma kujitosa katika vuguvugu hilo la Kiba. Nao wakaingia kuonesha ‘mahaba’ yao na kueleza jinsi walivyoguswa.

KIGWANGALLA ALIANZISHA…

Mbunge wa Nzega na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hamis Kigwangalla alikuwa kiongozi mkubwa wa serikali kuonyesha hisia zake katika kibao hicho kwani kupitia akaunti yake katika mtandao wa Twitter, aliandika:
“Seduce me dada…seduce me like what the hell…’ It’s simply a sing along…Congrats King.”

Baada ya Kigwangalla kuachia posti hiyo, wakafuata viongozi wengine, wakiwemo wabunge ambao nao walijitosa kumpongeza mwimbaji huyo kwa kibao hicho safi ambacho kinatikisa nchi kwa sasa. PROFESA JAY Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule ‘Profesa Jay’ naye aliguswa na Kiba, bila hiyana akajikuta ametupia kwenye mtandao wa Instagram; “This is what we call CLASSIC Material.. Big up to my young brother @ officialalikiba”

RIDHIWAN AIBUKA

Vurugu zilikuwa si za nchi hii, kwani Mbunge wa Chalinze, Ridhiwan Kikwete naye akaona isiwe tabu, asiidhulumu nafsi yake kwa kunyamaza wakati muziki mzuri umepenya kwenye moyo wake. Akaandika haya katika ukurasa wake wa Instagram: “@officialalikiba mdogo wangu hongera sana. Yaani nimetulia hapa nahisi kama unaimba kichwani mwangu. Keep the good Music Alive. Umefanikiwa #SeduceMe Kipusa, umefanikiwa kutupotosha #SeduceMe”

Ridhiwan Kikwete.
Wabunge wengine walioonyesha kuguswa na kibao hicho ni pamoja na Mbunge wa Sengerema na Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Mbunge wa Nzega, Hussein Bashe ambaye aliweka wazi kuwa licha ya yeye kuwa muumini wa Hip Hop, lakini amekunwa na kibao hicho.

HUYU HAPA PAUL MAKONDA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kupitia ukurasa wake wa Instagram, alitupia video ya Kiba na kuandika: “Tofauti zenu mimi nazipenda kwani zinaleta ushindani mzuri kwenye muziki. Ila naomba mzingatie sheria na utamaduni wetu.” ALI

HAPI HAKUBAKI NYUMA

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi naye hakuwa nyuma. Akatupia kipande cha video ya Seduce Me kisha akasindikiza na ujumbe uliosomeka: “Nimekuelewa sana wajina @officialalikiba. Kazi imeenda shule. Nidai zawadi kwa muziki huu wa ukweli, keep the fire burning.” MASTAA SASA Mbali na viongozi hao wa serikali na wananchi, vurugu zaidi mitandaoni ilifanywa na mastaa


mbalimbali wa filamu wakiwemo, Wema Sepetu, Jokate Mwegelo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Jacqueline Wolper. Kwa nyakati tofauti, kila mmoja alitupia video akionesha hisia zake kwa wimbo huo. Wema, Lulu na Jokate, wao walijirekodi vipande vya video wakitembea na kuonesha maumbo yao waliyojaaliwa na Mungu huku kwa mbali ikisikika Seduce Me kisha kuzitupia Instagram. Wolper naye aliutaja wimbo huo katika ukurasa wake wa Instagram kama ishara ya kuguswa na ngoma hiyo.

MENEJA WA KIBA ANENA

Risasi lilizungumza na mmoja wa mameneja wa Kiba, Aidan Seif ambaye aliwashukuru viongozi wote waliojikuta wameguswa na hiyo kali na ‘kuchafua’ kurasa zao za mitandao ya kijamii. “Tunaamini katika kufanya muziki mzuri na siyo jambo lingine lolote. Unapofanya kazi nzuri unategemea kupata mapokezi mazuri, tunashukuru Mungu na pia wadau na mashabiki wa kazi zetu.

Viongozi wetu tunashukuru kwa kuipokea Seduce Me na kuisapoti kadiri walivyoweza. Mungu awabariki, kwa niaba ya Kiba tunawashukuru sana na tunatoa ahadi ya kuendelea kufanya kazi nzuri kukuza sanaa yetu,” alisema Aidan. Mpaka tunakwenda mitamboni, wimbo huo tayari ulikuwa umeshatazamwa na watu 2,347,914 (milioni mbili na laki tatu na ushee) hivyo hadi leo, wimbo huo unatarajiwa kuwa umeshafikia watazamaji milioni tatu katika YouTube
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post