KISA MKWANJA WA MUMEWE MPYA, NAWAL AAMUA KUFUTA TATTOO YA NUH!

Baada ya Jini Mkatakamba kuipitia ndoa ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda, aliyekuwa mkewe Nawal amefunguka kuwa yupo katika harakati za kuifuta tattoo ya Nuh aliyoichora mkononi mwake.
Nawal ambaye baada ya kuachana na mzazi mwenziye Nuh Mziwanda, ameolewa tena na mwanaume anayefahamika kwa jina la Masoud, amefunguka Kwa kusema; “Nitaifuta tattoo ya Nuh Mziwanda, mume wangu ana fedha, atanipa ili niende kuifuta.”
Nawal na Nuh Mziwanda.
TUJIKUMBUSHE KIDOGO
Baada ya kutemana na Shilole, Nuh Mziwanda aliingia katika uhusiano wa kimapenzi na Nawal  ambapo Novemba, 2016,  walifanikiwa kufunga ndoa na wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kike anayeitwa Anyaghire.
Hivi karibuni ndoa yao ilivunjika baada ya kupitiwa na jini mkatakamba, kwa kile kinachodaiwa kuwa Nuh amerudi katika dini yake ya Kikristo na kwa kufanya hivyo ni kama amemkana mkewe aliyemuoa kwa dini ya Kiislamu, ambapo baada ya kutengana kwao, Nawal akaolewa tena na mwanaume anayefahamika kwa jina moja la Masoud.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post