KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA SARE ZA JWTZ ZENYE THAMANI YA ZAIDI YA MILIONI 50

Mfanyabiashara wa Kariakoo jijini Dar es salaam, Casto Onyomolile Ngogo (35) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu shtaka la uhujumu uchumi baada ya kukukutwa na sare 5,070 ambazo ni suruali, fulana na viatu vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Wakili wa Serikali, Wankyo Simon, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alisema kuwa Casto Ngogo, mkazi wa Tabata Segerea mkoani Dar es salaam, alikutwa na vifaa hivyo katika maeneo ya bandari kavu ya Galco Inland Container iliyoko Sokota, Chang’ombe Juni 15, 2017.
Wakili Simon alidai kuwa siku hiyo ya tukio, mshtakiwa alikutwa na suruali 5000 za JWTZ zenye thamani ya shilingi milioni 50 ambazo zimapatikana kwa njia isiyo halali. Pia alikutwa na fulana 50 za JWTZ zenye thamani ya shilingi 500,000 na jozi 20 za viatu vya jeshi hilo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post