KOREA KASKAZINI YATHIBITIKA KUWA NA UTAALAMU WA KUTENGENEZA MABOMU YA NYUKLIA

Ripoti ya upelelezi wa siri uliofanywa na Serikali ya Marekani imebainisha kwamba Korea Kaskazini kwa sasa imefanikiwa kupata teknolojia itayowawezesha kutengeneza mabomu ya nyuklia ambayo ni madogo sana yanayoweza kuwekwa kwenye makombora yaliyojaribiwa hivi karibuni.
Jumuia ya wapelelezi “wamesema kwamba Korea Kaskazini imetengeneza silaha za nyuklia zinazolenga kutumika kwenye makombora yao, ambayo baadhi yao yanaweza kuwekwa kwenye makombora daraja la ICBM (Inter Continental Ballistic Missile) – ambayo ni makombora ya masafa marefu yanayoweza kurushwa kutoka bara moja kwenda jingine.
Watafiti kwa muda mrefu walikuwa wakiishuku Korea Kaskazini kuwa inaweza kutengeneza vifaa vidogo vinavyoweza kubeba nyuklia vitavyoweza kuwekwa kwenye makombora hayo ya masafa marefu, lakini hii ndiyo nyaraka ya kwanza kutoka serikalini kuthibitisha kwamba nchi ya Korea Kaskazini inayo teknolojia hiyo.
Mwezi Machi mwaka 2016, Mtawala wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un alizungumza mbele ya vyombo vya habari kwamba wataalamu wa nchi yake wameweza kutengeneza mabomu ya nyuklia yanayokaa kwenye vifaa vidogo, lakini wachambuzi wa Marekani walishuku kwa kusema kuwa Korea Kaskazini haina teknolojia inayowawezesha kutengeneza mabomu hayo.
Habari hii mbaya imekuja wakati nchi ya Korea Kaskazini imeongeza kasi kubwa sana katika programu yake ya utengenezwaji wa makombora ambapo kwa mwezi Julai pekee ilifanya kwa ufanisi majaribio mawili ya kurusha makombora ya masafa marefu yenye uwezo wa kutoka nchini humo na kutua Marekani.
Rais wa Marekani, Donald Trump amekuwa akiiangalia Korea Kaskazini kwa karibu sana na amefanikiwa kuyashawishi mataifa 15 yaaliyo kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) kukubaliana kwa pamoja kuiwekea vikwazo Korea Kaskazini.
Hata hivyo, pamoja na vikwazo hivyo, wataalamu wa masuala ya silaha wanakubali kwamba vikwazo hivyo walivyowekewa Korea Kaskazini haviizuii nchi hiyo kuendelea kutengeneza makombora mengine na inaelekea kwamba sasa Marekani inabidi kushawishi kamati za usalama za kudhibiti nyuklia duniani kuweza kuifanya Korea Kaskazini iache kuendelea na uzalishaji huo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post