M PAWA YAKOPESHA BILIONI TANO KWA MWEZI

Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom kupitia bidhaa yake ya M-Pawa sasa inatoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni tano kwa mwezi kwa wateja ambao wana akaunti za M Pesa.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom, Rosalynn Mworia, huduma ya M-Pawa sasa inahudumia wateja takribani milioni tano nchini kote na ni miongoni mwa huduma zinazokua kwa kasi kubwa hapa nchini kwa sasa.
“Wateja wa Vodacom wenye akaunti ya M –Pesa wameanza kufaidika kwa wingi na huduma ya M-Pawa ambapo hupata huduma za kuhifadhi fedha zao na pia kupata mikopo pale wanapohitaji.
“Kwa ujumla, kiasi cha amana kilichopo katika mfumo wa M-Pawa kwa sasa kinafikia kiasi cha shilingi bilioni 15 huku shilingi bilioni tano zikikopeshwa kwa wateja wa kampuni yetu kila mwezi,” alisema Mworia.
Huduma ya M – Pawa ambayo hutumiwa na wateja wa M Pesa imekuwa kichocheo kikubwa katika ukuaji wa kasi wa idadi ya Watanzania ambao wanaweza sasa kufikiwa na huduma za kibenki kutoka popote pale walipo hapa nchini.
Alisema huduma hiyo ya M-Pawa imekuwa kimbilio la wengi kwa sababu masharti ya kuingia ni nafuu na mteja hapati usumbufu wa aina yoyote pale anapotaka kuweka fedha zake au kuomba mkopo kupitia akaunti yake ya M Pesa.
Akaunti ya M- Pawa maana yake ni akaunti ya benki iliyowekwa na mteja kwenye benki na ambayo imefunguliwa na kuendeshwa kwa mujibu wa kanuni na masharti yaliyopo.
Ili kufungua akaunti ya MPawa kwenye benki, ni lazima mtu angalau awe na umri wa miaka 18, amesajiliwa na uliyejiunga na kutumia vema huduma ya M-Pesa.
Kwa mujibu wa Mworia, mtu anaweza anaweza kufungua akaunti ya M-Pawa kwa kutuma maombi ya kieletroni tu yanayofanywa na mteja binafsi kwa kutumia simu yake kupitia menyu ya M-Pawa ambayo tayari ipo katika mfumo wa M-Pesa.
Mworia alisisitiza kwamba mtu anayetaka kujiunga na M-Pawa pia ni lazima akubali kuweka wazi taarifa zake binafsi ikiwa ni pamoja na namba ya simu, jina, tarehe ya kuzaliwa, namba ya utambulisho au ya pasipoti na taarifa nyingine ambazo zitaiwezesha benki kukubaini na kuendana na kanuni ya kumjua mteja wako na masharti ya kuzuia utakasaji wa fedha.
Kwa ujumla, kuna aina mbili za akaunti ya M Pawa kwa mteja wa Vodacom; moja ikiwa ni akaunti ya amana ambako mteja atakuwa akihifadhi fedha zake na akaunti ya mkopo kwa ajili ya kukopa wakati wa kuhitaji kufanya hivyo.
Kupitia akaunti ya amana, mteja anaweza kuhamisha fedha kutoka kwenye akaunti yake ya M-Pesa na/au kuchukua fedha kwenye akaunti yako ya M-Pesa.
Mmiliki wa akaunti ya M-Pawa, anaweza kuweka au kuchukua fedha kwenye akaunti yake ya amana ya M-Pesa kwa kutumia menyu ya M-Pawa kwa kutumia simu yake ya mkononi.
Kupitia utaratibu huo, ada ya muamala inayolipwa kwa Vodacom kwa ajili ya miamala iliyofanywa kwenye akaunti ya mteja wa M-Pesa siku hadi siku itatumiwa kwenye miamala yoyote itakayotekelezwa kwenye akaunti yake ya M-Pawa kwa kutumia mfumo wa M-Pesa.
Katika akaunti ya mkopo, mteja wa M- Pawa anaweza kukopa kwa kiwango cha chini cha shilingi 1,000 na kiwango cha juu cha shilingi laki tano za Kitanzania kulingana na kutimiza vigezo na masharti vilivyowekwa. Mapato ya mkopo huo kwa mteja yataingizwa kwenye akaunti yake ya M-Pesa baada ya makato ya ada za mumala uliotumika katika akaunti kufanyika. Mkopo huo hutakiwa kulipwa ndani ya siku thelathini.
Mwisho
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post