MAGUFULI AMPA MWEKEZAJI ARDHI KIJIJINI KWA RAIS KIKWETE

Jonas Kamaleki- MAELEZO
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameridhia mwekazaji kupewa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda kijijini Msoga, Wilayani Chalinze, Mkoa wa Pwani.
Waziri Lukuvi amesema kuwa wanakijiji wana uwezo wa kutoa ardhi hadi ekari hamsini tu, zaidi ya hapo ni  Rais ndiye mwenye uwezo wa kutoa hati kwa mwekazaji, hivyo alikwenda Msoga kujiridhisha kabla ya kumshauri  Rais kutoa hati kwa mwekezaji.
Aliwauliza wananchi katika mkutano uliofanyika kijijini Msoga kama walikubaliana kumruhusu mwekazaji wa Region Recycling East Africa Limited kujenga kiwanda kijijini hapo, nao wananchi kwa pamoja walisema kuwa ndiyo walitoa ardhi yao kwa ajili ya uwekezezaji huo.
Kiwanda hicho kitakuwa kinatumia betri mbovu za gari na za umeme jua  (Recycling) kama malighafi ya kutengeneza betri nyingine kwa ajili ya matumizi ya magari na mitambo ya umeme jua. Mwekezaji huyo alipewa jumla ya ekari 56 na wanakijiji wa Msoga kwa ajili ya uwekezaji huo.
“Vijiji vilivyopimwa kimji vitaiingizia Serikali mapato na wananchi pia watapata fursa za kupata mikopo kwenye mabenki na kufanya biashara kubwa,” alisema Lukuvi na kuongeza kuwa anazishauri Halmashauri zote nchini kupandisha hadhi vijiji vya namna hiyo.
Kwa upande wake, Mbunge wa Chalinze,  Ridhiwan Kikwete alimshukuru Lukuvi kwa kuridhia umilikishwaji wa ardhi kwa mwekezaji kwani kiwanda hicho kikianza kazi kitatoa fursa mbalimbali zitakazochangia kuinua uchumi wa wakazi wa Msoga na maeneo ya jirani ikiwemo ajira.
Alimwomba Waziri Lukuvi kupitia wizara yake kuwasaidia katika upimaji wa maeneo ya Chalinze kwani wao hawana uwezo wa kujipimia au kulipia gharama za upimaji.
Hatua za umilikishwaji ardhi kwa mwekezaji huyo, zilianza mwaka 2012 na kukamilika hivi karibuni kwa jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano ambayo imekuwa karibu sana na wananchi kuwatatulia kero na changamoto mbalimbali.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi chini ya uongozi wa William Lukuvi imetatua migogoro mingi ya ardhi hapa nchini na kuwafanya wananchi waishi kwa Amani katika maeneo yao.
Mwisho
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post