MAJIBU YA SERIKALI KUHUSU HOJA YA KUSHIKILIWA WA NDEGE YAKE CANADA

Serikali imesema kuwa ni kweli kwamba kuna mgogoro katika ununuzi wa ndege mpya ya tatu ya serikali aina ya Bombardier Q400 Dash 8 Nextgen nchini Canada na kwamba taratibu za kidiplomasia na kisheria zimeanza kuchukuliwa kumaliza mgogoro huo.
Aidha, imeelezwa kuwa, mgogoro katika utengenezaji wa ndege hiyo umesababishwa na wanasiasa na watu wasioitakia mema Tanzania ambao wanataka ishindwe kuwaletea wananchi maendeleo.
“Ununuzi wa ndege ya 3 ya Bombadier umeingiliwa na mgogoro uliotengenezwa na wanasiasa na watu wasioitakia mema Tanzania, Wanasiasa waliotengeneza mgogoro huo wanahujumu maendeleo ya nchi na usalama wa raia.”
Hayo yote yamesemwa leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa ambapo aliwatoa wananchi hofu kwa kusema kuwa ndege hiyo itawasili nchini na kwamba waiamini serikali yao.
Kawawa amelazimika kutoa ufafanuzi huo kufuatia taarifa iliyotolewa jana na  Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu kuwa ndege hiyo imekamatwa nchini Canada.
Katika taarifa yake, Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki alisema wadeni wa taifa wameishikilia ndege hiyo iliyokuwa iwasili nchini Tanzania mwezi Julai. Lissu alisema Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Mahiga alikwenda Canada kujaribu kuzungumza na wadeni hao ili waiachie ndege hiyo.
Zaidi, Lissu alihoji kuwa serikali inaficha taarifa hizo kwa faida ya nani kwani Waziri wa Ujenzi, Prof. Mbarawa alipoulizwa na Mbunge wa Kigoma Mjini kuhusu kuchelewa kwa ndege hiyo alisema kuna taratibu hazijakamilika lakini itakuja. Alipotakiwa kusema ni taratibu gani hazijakamilika, Waziri Mbarawa hakujibu.
Kawawa akipangua taarifa hizo alisema “Ndege ya 3 ya Bombadier ipo na inakuja kwahiyo wananchi waiamini Serikali yao, ila serikali imesikitishwa na ushiriki wa wanasiasa na baadhi ya watu kuhujumu maendeleo ya nchi. Watanzania tuwe wazalendo kulinda, kutetea na kukabiliana na hujuma zozote zinazorudisha nyuma maendeleo ya Nchi. Tuunge mkono jitihada za Rais Magufuli  katika kuleta maendeleo bila kujali itikadi ya chama, kabila au dini.”
Tanzania inapanga kununua ndege aina ya Boeing 787 Dash 8 Dreamliner yenye uwezo wa kuchukua abiria 262 ambayo inatarajiwa kuwasili nchini humo Juni 2018.
Ndege nyingine ambazo Tanzania itazinunua ni ndege moja aina Bombardier Q400 Dash 8 NextGen ambayo ndiyo yenye mgogoro, ndege 2 aina ya Bombardier CS300 zenye uwezo wa kuchukua kati ya abiria 137 na 150 na zinazotarajiwa kuwasili nchini kati ya Mei na Juni, 2018.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post