MAKAMU WA RAIS AWASILI AFRIKA KUSINI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasili nchini Afrika Kusini leo mchana tayari kwa kuhudhuria mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika ( SADC).
Makamu wa Rais anahudhuria mkutano huo ulioanza tarehe 9 Agosti, utaendelea mpaka tarehe 20 Agosti akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Katika mkutano huo, Mwenyekiti wa  Jumuiya hiyo, Mfalme Mswati III wa Swaziland akiwa anatoa ujumbe wake wa siku amesema kwamba anaamini kwamba agenda ya SADC kuhusu muungano na maendeleo itafanikiwa.
Tarehe 17 ya mwezi Agosti kila mwaka, nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika ( SADC) wanasherehekea siku hiyo kufurahia maendeleo yaliyofikiwa na jumuiya tangu kuanzishwa kwake tarehe kama ya leo mwaka 1992.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post