MAKONDA AIZUIA WIZARA KUBOMOA NYUMBA DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amezuia kufanyika kwa operesheni ya kubomoa nyumba zaidi ya 17,000 katika Bonde la Mto Msimbazi kutokana na wahusika waliopanga kufanya kazi hiyo kutofuata taratibu.
Akizungumza leo na wananchi pamoja wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Makonda amesema kuwa alishangaa kusikia taarifa za kubomolewa kwa nyumba 17,000 ndani ya mkoa anaouongoza bila yeye kupewa taarifa za mpango huo.
Makonda amesema kwamba, Rais Magufuli alimuuliza kama alikuwa na taarifa na ubumoaji huo uliotangazwa na Baraza la Mazingira la Taifa na Wizara ya Ardhi, akasema hakuwa na taarifa, na Rais hana taarifa zozote, na hivyo kwa vile wahusika wameshindwa kufuata taratibu, amesitisha mpamgo huo.
“Rais aliniuliza kama nina taarifa za bomoabomoa hii ya Bonde la Msimbazi, nikasema sina na yeye akasema hana taarifa hizo. Kwa sababu hawajafuata utaratibu nasitisha ubomoaji wa nyumba Dar es Salaa kuanzia sasa,” alisema Makonda.
Kuhusu ubomoaji unaoendeshwa na TANROADS pamoja na RAHCO katika maeneo mengine, Makonda alisema hao wanaweza kuendelea kwa sababu walitoa taarifa.
Kuhusu bomoabomoa hiyo iliyozuiwa leo, awali Ofisa Mipango Miji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Charles Mkalawa aliyeambatana na Mwanasheria Mwandamizi wa Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi ya Mazingira (NEMC), Heche Suguti alisema nyumba hizo ni miongoni mwa zilizowekewa alama ya X katika bomoabomoa iliyositishwa mwaka jana.
Dk Mkalawa alisema hakuna mwananchi atayelipwa fidia katika mchakato huo na kwamba wangeweza kulipwa endapo eneo hilo lingekuwa bado halijaandaliwa mpango wa kuliendeleza.
“Kisheria mvamizi wa eneo husika hatakiwi kupewa taarifa, badala yake unakwenda kumtoa moja kwa moja. Lakini Serikali imekuwa ya kistaarabu na yenye huruma na inawabembeleza kwa kuwapa taarifa za kuondoka,” alisema Mkalawa
Aidha, wakati huo huo Makonda ametangaza kuwa, Rais Dkt Magufuli amesitisha zoezi la ubomoaji wa nyumba zilizojengwa katika Bonde la Toangoma jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wakazi wa maeneo hayo mapema leo, Makonda amesema kwamba alikubaliana na Rais kwamba wakazi hao wajenge vizuri bila kukiuka taratibu na kwamba hakuna atakayebomolewa.
Makonda amemuagiza Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa kumkamata mtu yeyote atakayeendesha zoezi la kubomoa nyumba bila kutoa taarifa.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post