MAKONDA NA RUGE WAKUBALIANA KUWEKA CHINI SILAHA ZAO

Jana Agosti 9, 2017 Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limetangaza kuondoa zuio la kutotangaza habari za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Mkonda jijini Dar es Salaam baada ya kufanya mazungumzo baina ya pande zinazohusika.
Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Theophil Makunga wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ambapo alifafanua kwamba, mgogoro uliokuwepo kati ya tasnia ya habari  na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Mkonda umefika mwisho hivyo wanarusu sasa habari zake ziandikwe tena na vyombo vya habari baada ya kutofanya hivyo kwa takribani miezi 5.
Itakumbukwa kuwa, Machi 22 mwaka huu Jukwaa la Wahariri lilitoa tamko lililokuwa likivitaka vyombo vya habari kususia habari za kiongozi huyo wa mkoa kufuatia madai yaliyokuwepo ya kuvamia kituo cha Clouds Media Group na kushinikizwa kurushwa kwa kipindi ambacho hakikuwa kimetayarishwa kikamilifu.
Aidha, Mkuu wa Mkoa alisema kwamba hawezi kamwe kuomba msamaha kwa tukio lililotokea kwa sababu uamuzi huo ulitolewa bila kusikilizwa kwa pande zote huku akisisitiza kwamba hakuvamia ofisi za Clouds kama inavyodaiwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba amesema kwamba mgogoro huo ni lazima sasa ufikie mwisho kutokana na Rais Dkt Magufuli kuwaita mbele ya umati wa watu na kuwataka wapatane.
Akitolea mfano wa dereva wa lori uliowahi kutolewa na Rais Magufuli, Ruge alisema kwamba dereva amewataka abiria waliopo kwenye lori kuacha kulumbana kwani migogoro yao huenda ikapoteza muelekeo wa lori.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post