MAMBO MANNE USIYOYAJUA KUHUSU MCHAKATO WA AJIRA

Afisa rasilimali-watu mstaafu mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 15 ameelezea uzoefu wake mambo yanayotokea kwenye mchakato wa kuajiri kwenye kampuni au taasisi mbalimbali. Mbinu zinazotumiwa na kampuni au taasisi hizi kupata watu inaoweza kuwaajiri – na si mara zote inafata taratibu zilizowekwa kama ambavyo ungetegemea.
Maafisa waajiri wapo tayari kufanya mambo mengi sana (mengine huwezi kuyatarajia) ili waweze kupata mwajiriwa sahihi kwa nafasi iliyopo.
Unadhani waajiri hawaangalii akaunti zako za mitandao ya kijamii? Au labda kuwa na watoto hakuna athari yoyote katika kuongeza au kupunguza uwezekano wako wa kupata ajira ya ndoto zako?
Fikiria upya!
Zifuatazo ni baadhi tu ya mbinu wanazotumia kuajiri wafanyakazi mbalimbali ambazo watu wengi hawajui:
1. Wanapitia (kwa umakini) historia yako
Hii huwa haisemwi lakini waajiri ni lazima watawasiliana na wadhamini wako ili kuthibitisha kama watu na mambo uliyoandika kwenye wasifu wako ni sahihi. Lakini kuchunguza mtu kabla ya kumuajiri kunaenda mbali zaidi ya hapo.
Maafisa waajiri ni wachache na ingawa sio utaratibu unaotakiwa, wengi wanapigiana simu kwa afisa rasilimali-watu wa kampuni au taasisi uliyowahi kufanya kazi kabla, lengo likiwa ni kupata taarifa zako zisizo rasmi kuhusu utendaji kazi wako, jinsi ulivyo na mengine mengi. Wanapata taarifa za ndani kabisa – kutoka kwa mtu wanayemuamini ambaye hayupo kwenye orodha ya wadhamini wa muombe kazi. Mara nyingi maafisa waajiri wa sehemu uliyowahi kufanya kazi wakikuzungumzia vizuri, basi unapita bila kipingamizi kwenye ajira unayoitaka sasa.
Njia nyingine nzuri na rahisi sana inayotumiwa sasa na maafisa waajiri ni kupitia mitandao ya kijamii, hasa kupitia mtandao wa LinkedIn.
Baada ya kupitia watu walio kwenye mtandao wako kupitia LinkedIn, maafisa waajiri huwa wanakuwa na wasiwasi juu ya watu wasiokuwa na mtandao wa kutosha wa watu wanaojihusisha na sekta unayoomba kazi na wengi wataona kama umejisifu kupita kiasi kwenye wasifu wako, lakini si mzoefu wa taaluma uliyoimbea kazi.
Bila shaka, kuwa makini na mambo unayoweka kwenye akaunti zako za mitandao ya kijamii si jambo linalohitaji akili sana. Kuna baadhi ya mameneja wanaochunguza akaunti za wafanyakazi wao kuona kama wamekuwa wakizungumzia vibaya kampuni hiyo.
2. Una mtoto/watoto?
Ingawa ni kinyume cha Sheria kwa muajiri kuzingatia familia ya mtu wakati wa kuajiri, hii haimaanishi kwamba jambo hili halifanyiki. Huwezi kuzuia maswali yanayoweza kuwa yanapita kichwani kwa muajiri. (“Huyu ataweza kufanya kazi yetu kwa ufanisi ikiwa mtoto anaumwa nyumbani?”)
Utapojikuta umeulizwa swali kama: Nini unapenda kufanya siku za mapumziko ya mwisho wa wiki? Ujue muajiri anataka kujua kama una watoto au la!
Kwa kujua kwamba waajiriwa wapya wanatakiwa kufanya kazi kwa muda mrefu, waajiri wanajua kwamba kuwa na watoto kutafanya waajiriwa kutoweza kufanya hivyo—na ni mara chache watahudhuria kwenye sherehe za kazini.
Waajiri wengi (hasa ambao si wanasheria) watahakikisha kwamba mtu anayeajiriwa anaendana na utamaduni wa kampuni hiyo — mtu atakayekuwa mfanyakazi na rafiki mzuri pia.
Na mara nyingi kama mwanamke atafanya usaili akiwa mja mzito, ni bora asiseme lolote kuhusu hilo mpaka atakapoajiriwa rasmi kwakuwa waajiri wengi wanaweza kuitumia fursa hiyo kukuondoa kwenye orodha ya watu wanaofaa.
3. Unaweza kulipwa pesa zaidi ya uliyotajiwa
Katika mchakato wa kuajiri, majadiliano ya mshahara utakaolipwa hayaepukiki lakini mameneja wengi wanaweza kukulipa pesa nyingi zaidi ya mshahara wanaousema mwanzo.
Bila shaka wanaweza wakawa wagumu kuongeza mshahara wako kwakuwa sera za malipo ya mshahara zina viwango maalum—mara nyingi mameneja wanajua kiwango cha mshahara watakaokulipa hata kabla hujafanyiwa usaili. Lakini wanaweza kukuidhinishia marupurupu mbalimbali yatakayofidia kiwango ulichokiomba.
Mameneja wanapenda kutoa marupurupu na bonsai kwakuwa havionekani kwenye karatasi ya malipo ya mshahara na waajiri huwa wanaidhinisha marupurupu haya mara moja kama wakiona una umuhimu kwao na dalili zinaonesha hujavutiwa na kiasi cha mshahara wao.
Kikubwa, na si jambo la kushangaza, ni kutambua kwamba waajiri hawawezi kukuomba wakupe bonsai au marupurupu. Ni jukumu lako wewe unayefanyiwa usaili kuulizia.
Swala la kuulizia marupurupu litafanya wakuone wa thamani kubwa kuliko kung’ang’ania kuongezewa mshahara (kwakuwa mshahara hauwezi kuongezeka zaidi ya sera za kampuni zinavyotaka). Hata hivyo, hii haimaanishi kwamba usijadili kabisa kuhusu mshahara wako—lakini unatakiwa kumshawishi muajiri kwanini unastahili kuwa katika kundi la watu wachache wanaolipwa zaidi na kampuni hiyo.
4. Unaweza kukubaliana na bosi wako kwamba uache kazi
Kama muajiriwa anaacha kazi mwenyewe— asiwe ameachishwa au kupunguzwa — kampuni hailazimiki kumlipa chochote, si kiinua mgongo wala stahiki zake, kwakuwa ameacha kazi mwenyewe. Kwahiyo, likizingatiwa swala la fedha, kampuni zote zinapenda wafanyakazi isiowataka waache kazi wenyewe ili isiwalipe fidia ambayo ilitakiwa iwalipe kama wangefukuzwa.
Je, mameneja wanaweza kufanya makusudi kuhakikisha wafanyakazi wasiowapenda wanaacha kazi? Huwa inatokea sana — lakini huwa inafanywa na mameneja halafu maafisa waajiri huwa wanataarifiwa baada ya uamuzi huo.
Kimsingi, kampuni huwa zinaruhusu wafanyakazi kuondoka kwa makubaliano maalum. Mfanyakazi anaweza akahitajika kubaki mpaka tarehe fulani au mpaka amalize kazi fulani, au kwa makubaliano kwamba akiondoka asichukue wafanyakazi wa kampuni hiyo na kisha baada ya makubaliano hayo, atalipwa kiasi fulani cha pesa kwa ajili ya kumfanya atimize alichoahidi.
Malipo haya huwa yanajulikana kama malipo ya kuachana, na huwa hayahesabiwi kama ni kiinua mgongo au fidia. Makubaliano haya hufanywa mara nyingi sana kimyakimya.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post