‘MASOGANGE’ ANA KESI YA KUJIBU DAWA ZA KULEVYA

Video Queen, Agnes Gerald ‘Masogang aliyevaa gauni la kijani aikitoka mahakamani kusikiliza kesi inayomkabili.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema kuwa Video Queen, Agnes Gerald ‘Masogange’, anayo kesi ya kujibu kwa kudaiwa kutumia dawa za kulevya, hivyo anapaswa kujitetea.
Kesi hiyo ambayo imeunguruma leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, amesema kuwa amekubaliana na hoja za ushahidi wa upande wa mashtaka ambapo mshtakiwa amekutwa na kesi ya kujibu na hivyo ana haki ya kujitetea.
Baada ya kauli ya hakimu huyo, Masogange amesema atajitetea kwa njia ya kiapo na atakuwa na mashahidi watatu. Hakimu Mashauri ameiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 12, mwaka huu ambapo mtuhumiwa ataanza kujitetea.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post