MATUKIO 7 YALIYOMWENDEA KOMBO TRUMP KWA MWEZI ULIOPITA

SHARE:

Kwa Wamarekani wengi, wiki nne zilizopita zilikuwa na misukosuko mkubwa kwa Rais wa nchi hiyo, Donald Trump na kusababisha takwimu za kuk...

Kwa Wamarekani wengi, wiki nne zilizopita zilikuwa na misukosuko mkubwa kwa Rais wa nchi hiyo, Donald Trump na kusababisha takwimu za kukubalika kwake na wananchi kuporomoka zaidi tofauti na marais wote waliowahi kulitawala Taifa hilo, mbaya zaidi akilinganishwa na mtangulizi wake ambaye aikuwa akikubalika sana.
Upepo wa kujiuzulu, kuajiri na kufukuza mara kwa mara wasaidizi wa ngazi za juu ulikuwa ndio wimbo wa kila siku kwenye vyombo vya habari vya nchi hiyo kwa zaidi ya mwezi mmoja uliopita. Ingawa sio kila habari ilisababishwa moja kwa moja na Rais Trump mwenyewe, hali hiiinaashiria kwamba upepo ndani ya Ikulu ya nchi hiyo si mzuri.
Haya ni baadhi ya matukio yaliyoichanganya Serikali ya nchi hiyo kwa wiki nne zilizopita:

Mabadiliko makubwa ya wafanyakazi wa Ikulu

Kufukuzwa kazi kwa wasaidizi wa karibu wa Trump si jambo jipya tangu kuanza kwa utawala wa Rais huyo, lakini kuongezeka kwa kufukuzwa kwa wasaidizi wa ngazi za juu kabisa kwa wiki nne zilizopita zimetangazwa sana kwenye vyombo mbalimbali vya habari.
Sean Spicer alikuwa msemaji wa Ikulu mwenye mahusiano mabaya sana na vyombo vya habari, alijiuzulu Julai 21 baada ya kuenea kwa tetesi kwamba alikuwa akipinga vikali uamuzi wa Rais Trump kumteua Anthony Scaramucci kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu.
Baada ya siku chache tu tangu kujiuzulu kwa Spicer, Mkuu wa Utawala wa Ikulu Reince Priebus akafukuzwa kutokana na taarifa kwamba alikuwa katika uhusiano mbaya na Scaramucci. Priebus alifukuzwa na Scaramucci ambaye alimlaumu kwa kuvujisha taarifa kwa vyombo vya habari.
Baada ya siku kumi tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo, Scaramucci naye akafukuzwa kazi ikiwa ni baada ya mahojiano aliyofanya na kituo cha The New Yorker baada ya kuwakashifu wasaidizi wa karibu wa Rais huyo.
Baada ya kuondoka kwa Spicer, Priebus, na Scaramucci, Rais Trump akamteua aliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani, John Kelly kuwa Mkuu wa Utawala wa Ikulu.
Siku ya Ijumaa ya Agosti 18, Mkuu wa Idara ya Mipango ya Ikulu, Steve Bannon naye alijiuzulu nafasi yake.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ‘msumbufu’

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jenerali Jeff Sessions alimchokonoa Rais Trump kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la The New York Times Julai 19. Trump alilaumu uamuzi wa Sessions kujiuzulu kutokana na FBI kuendeleza uchunguzi wa Urusi kuingilia Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo uliofanyika mwaka 2016.
Akisema kwamba kujiuzulu huko “hakujamtendea haki Rais,” Trump alisema kwamba kama angejua endapo Sessions atajiuzulu, basi ange “teua mtu mwingine.”
Baada ya siku chache, Trump alimlaumu tena kupitia mtandao wa Twitter.
Watu wengi ndani ya chama cha Republican walimshambulia Trump baada ya kumlaumu Sessions ambaye alikuwa moja ya washirika wakubwa sana wa Trump na waliomuunga mkono katika kampeni za kutafuta urais mwaka 2016.

Kushindwa kwa mpango wa kuifuta Obamacare

Mpango wa zaidi ya miaka saba aliokuwa nao Trump kutaka kuufuta na kubadili mpango wa afya ulioanzishwa na mtangulizi wake Barrack Obama (maarufu kama Obamacare) uliangukia pua Julai 28 baada ya Bunge la Seneti la nchi hiyo kutupilia mbali muswada huo wa Trump baada ya kura nyingi kuukataa.
Baada ya matokeo ya kura hizo, Trump akawashambulia wabunge wa Seneti wa chama chake cha Republican kupitia mtandao wa Twitter akiwalaumu kwa “kuwaangusha wananchi wa Marekani,” na akashauri kuwepo kwa mabadiliko katika mchakato wa Bunge kupitisha maamuzi.

Wanajeshi waliobadili jinsia ambao bado wapo kazini

Wakati Waziri wa Ulinzi James Mattis alipokuwa likizo, Rais Trump alipendekeza mabadiliko makubwa kufanywa kuhusu wanajeshi waliobadili jinsia ambao bado wako kazini.
Agosti 9, Rais Trump alipendekeza kusitishwa kwa utaratibu uliowawezesha wanajeshi waliobadili jinsia kujiweka wazi ndani ya jeshi hilo, akisema kupitia akaunti yake ya mtandao wa Twitter kwamba jeshi “haliwezi kuelemewa kwa kubeba gharama kubwa za afya na usumbufu unaoletwa kutokana na wanajeshi waliobadili jinsia.”
Wabunge wengi pamoja na wanajeshi waliudhihaki msimamo na mapendekezo hayo ya Trump wakisema kwamba tafiti zilazofanywa zinaoneshwa athari ndogo sana inayotokana na askari waliobadili jinsia.
Kauli hii ya Trump ilizua mkanganyiko kwa viongozi wa ngazi za juu jeshini, Ikulu pamoja na Makao Makuu ya Wizara ya Ulinzi (Pentagon) kwakuwa wasomaji wa taasisi hizo wamekuwa katika wakati mgumu kuyatolea maelezo kauli hiyo ya Rais Trump.

Kupingwa kwa ombi lake la kutowahurumia wahalifu

Julai 28, Rais Trump alizungumza na maafisa wa polisi katika kitongoji cha Long Island jijini New York na kusema:
“Kwa pamoja tutarudisha usalama mitaani mwetu na amani kwenye jamii na tutausambaratisha mtandao wa genge la uhalifu la MS-13 pamoja na magenge mengine mengi,” alisema Trump.
Mazungumzo haya ambayo mwanzo yalionekana kama ya kuwahamasisha maafisa wa polisi hao ilibadili muelekeo ghafla baada ya Trump kutoa ushauri kuhusu jinsi polisi wanavyokamata watuhumiwa wa matukio ya uhalifu.
“Mnajua jinsi mnavyofanya kwa kulinda mtu asigonge kichwa chake mkiwa mnamuingiza ndani ya gari? Mnawalinda wasijigonge kichwani wakati labda unakuta ametoka kuua mtu — halafu nyinyi mnawalinda wasijigonge kichwani. Nasema kwamba hamna sababu ya kuwalinda wasijigonge,” Trump aliwaambia maafisa hao.
Maafisa hao wa Polisi walitoa kauli kujitenga na kauli hiyo ya Trump kwa kusema: “Kama polisi, hatuungi na hatutaunga mkono kuwakuwatesa wafungwa,” walisema katika kauli yao.

Swala la Urusi

Rais Trump alikutana na Rais wa Urusi, Vladimir Putin kwenye mkutano wa nchi tajiri zaidi duniani, G-20 Julai 7, 2017, jijini Hamburg – Ujerumani.
Baada ya Rais wa Urusi, Vladimir Putin kuiomba Marekani kupunguza wafanyakazi 755 wa Ubalozi wake uliopo Urusi na kubakiza wafanyakazi wachache, siku ya Agosti 10, Trump alijibu kwa kusema kuwa “amefurahia ” ombi hilo.
“Napenda nimshukuru kwakuwa tunajaribu kupunguza idadi ya wafanyakazi,” alisema Trump, akizungumzia ombi la Putin, “na kadri ya uelewa wangu, ninashukuru kwa kupunguza idadi kubwa ya wafanyakazi kwa sababu sasa tutakuwa na wafanyakazi wachache wa kuwalipa.”
“Hakuna sababu ya msingi ya wao kurudi (nchini Urusi),” alisema Trump. “Nafurahi kwa sababu sasa tunaweza kubaki na pesa tulizokuwa tukilipa mishahara. Tutaokoa fedha nyingi sana.”
Kauli hii ya Trump ilipingwa mara moja na viongozi wa vyama vya Republican na Democrat.
Siku kadhaa baadaye, Bunge la Congress likaweka vikwazo kwa Urusi ambapo pia vinafanya Trump asiwe na mamlaka ya kuvitoa. Rais Trump alitia sahihi uamuzi huo siku ya Agosti 2, lakini alisema kuwa kitendo hicho hakikuwa cha kikatiba.

Swala la mpaka wa Mexico

Trump alizungumza kwamba amepigiwa simu na Rais wa Mexico, Enrique Peña Nieto, ambaye alisema kuwa alimpongeza kwa sera zake za uhamiaji.
“Hata rais wa Mexico amenipigia simu,” alisema Trump kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri. “Aliniambia kwamba kwenye mpaka wa kusini mwa nchi yao, watu wachache sana wanakuja wakitaka kuvuka kwa sababu wamajua hawawezi kuvuka kwenye mpaka wetu, jambo ambalo ni mafanikio.”
Maafisa wa Serikali ya Mexican walikana kuhusu simu hiyo aliyoizungumzia Trump wakisema kwamba mara ya mwisho marais hao kuzungumza ilikuwa ni kwenye mkutano wa G-20 uliofanyika mwezi Julai.
Afisa Habari wa Ikulu, Sarah Huckabee Sanders aliitetea kauli hiyo ya bosi wake akisema kwamba mazungumzo kati ya wakuu hao yalifanyika walipokutana mara ya mwisho.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: MATUKIO 7 YALIYOMWENDEA KOMBO TRUMP KWA MWEZI ULIOPITA
MATUKIO 7 YALIYOMWENDEA KOMBO TRUMP KWA MWEZI ULIOPITA
https://1.bp.blogspot.com/-KrYzoJT635o/WZ6X1a-BkwI/AAAAAAAAd6k/bHj0gkEndf8IjDbw8qkOviTjD8GxMsY7gCLcBGAs/s1600/x81e7960ea6064fce31c1e41377f808c27d025b01d47c0873d85971c36c09f118_4074641-750x375.jpg.pagespeed.ic.iVFexJEQAa.webp
https://1.bp.blogspot.com/-KrYzoJT635o/WZ6X1a-BkwI/AAAAAAAAd6k/bHj0gkEndf8IjDbw8qkOviTjD8GxMsY7gCLcBGAs/s72-c/x81e7960ea6064fce31c1e41377f808c27d025b01d47c0873d85971c36c09f118_4074641-750x375.jpg.pagespeed.ic.iVFexJEQAa.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/08/matukio-7-yaliyomwendea-kombo-trump-kwa.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/08/matukio-7-yaliyomwendea-kombo-trump-kwa.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy