MKE WA RAIS MUGABE AWAFUMANIA WANAWE NA KUMSHAMBULIA MSICHANA ALIYEKUWA NAO

Mke wa Rais wa Zimbabwe, Grace Mugabe anatuhumiwa kumpiga na kumsabababishia majeraha madogo msichana mmoja aliyemkuta na wanawe wawili wa kiume mjini Johannesburg Agosti 13.
Grace Mugabe alikuwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya mguu.
Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Bulawayo 24 ya nchini Zimbabwe na jumbe mbalimbali zilizotumwa kupitia mtandao wa Twitter mjini Johannesburg na Harare, zimedai kuwa Grace Mugabe alimshambulia msichana aliyefahamika kwa jina la Gaby kwa kutumia waya wa umeme baada ya kumkuta na wanae wawili, Robert Jr (25) na Chatunga (21).
Watoto hao wawili ambao wapo mjini hapo kwa ajili ya shule, walikuwa hawawezi kusimama kutokana na kufanya sherehe kwa muda mrefu. Watoto hao wanafahamika kwa kula bata zaidi kuliko kusoma, kitu ambacho ndio lengo la wao kuwepo nchini humo.
Hivi karibuni Robert Mugabe Jnr, na Chatunga Bellarmine,  walifukuzwa katika nyumba waliyokuwa wakiishi eneo la Rivonia baada ya kusababisha usumbufu kutokana na kelele za muziki na watu waliokuwa wakija katika nyumba hiyo. Hata baada ya kufukuzwa, walitakiwa kuikarabati nyumba hiyo.
Msichana huyo aliyepigwa na Grace alipata jeraha kichwani kwake na kwamba walinzi walikuwa wakiangalia tu namna anavyoshambuliwa na mke huyo wa Rais wa Zimbabwe.
Msichana huyo alichapisha mtiririko wa jumbe kuhusu shambulio hilo;
Please don't come here with your ignorance. Check the hotel cameras.
Since you know them personally please find out your damn self! https://twitter.com/a_ajida/status/896981010495270912 


JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post