MKOJO WA WEMA SEPETU WAKUTWA UNA BANGI

SHARE:

Kesi ya matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi inayomkabili mrembo Wema Sepetu jana aliendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu M...

Kesi ya matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi inayomkabili mrembo Wema Sepetu jana aliendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo shahidi namba moja kwa upande wa mashtaka alitoa ushahidi wake na kusema kuwa mkojo wa mrembo huyo ulionyesha kuwa alivuta bangi.
Shahidi huyo, Elias Mulima kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali akiongozwa na wakili wa serikali Constantine Kakula aliieleza mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba namna alivyompima mtuhumiwa huyo na kubaini kuwa mkojo wake ulikuwa na bangi ambapo sampuli ya mkojo huo aliipokea Februari 8.
Shahidi alisema baada ya Wema kutoa sampuli ya mkojo huo ilipelekwa maabara ambapo lengo lilikuwa ni kuchunguza chembechembe za uwepo wa dawa za kulevya na ndipo walipobaini uwepo wa dawa za kulevya aina ya bangi. Baada ya kutoa ushahidi huo, Elias alitoa taarifa ya uchunguzi aliyoiandaa na kuisaini yeye mwenyewe na pia kuthibitishwa na kaimu mkemia mkuu wa serikali ili itumike kama kielelezo cha ushahidi.
Baada ya hoja hizo, upande wa utetezi unaoongozwa na Wakili Peter Kibatala aliitaka mahakama kutopokea taarifa hiyo kwa sababu uchunguzi haukufuata sheria kwani Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai inataka uchunguzi wa kitabibu kwa mtuhumiwa ambaye yupo chini ya ulinzi lazima upate kibali cha mahakama.
Aidha alitaka pia mahakama isipokee taarifa hiyo kwa sababu haikumbatanaishwa na fomu namba DCEA 001.
Akijibu hoja hizo, hakimu aliyekuwa mahakamani hapo alisema kuwa, fomu yenye namba 001 inatumiwa na Polisi wanaopeleka sampuli na fomu namba 009 ni taarifa ya mkemia, na kwamba fomu moja haitegemei nyingine kwa sababu huandaliwa na watu tofauti.
Hakimu pia aliipangua hoja ya Kibatala ya kibali cha mahakama ambapo alisema sheria haijasema kuwa wakati wote lazima Polisi waombe kibali hicho cha uchunguzi wa kitabibu, lakini pale ambapo mtuhumiwa atakuwa hayupo tayari, wanaweza kuomba kibali cha mahakama.
Kutokana na mvutano ulioibuka mahakamani hapo kuhusu taarifa hiyo ya uchunguzi, mahakama iliomba muda wa kupitia nyaraka hizo na kesi hiyo ikaahirishwa hadi Agosti 4 mwaka huu.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: MKOJO WA WEMA SEPETU WAKUTWA UNA BANGI
MKOJO WA WEMA SEPETU WAKUTWA UNA BANGI
https://1.bp.blogspot.com/-6WNws4M97OY/WYHEVriXAYI/AAAAAAAAdPY/_eNoowXoXZ8kADmPLndEEVaOhvPnVk4aQCLcBGAs/s1600/xDGJB0UUXoAAHCvv-750x375.jpg.pagespeed.ic.WqQj0SWivJ.webp
https://1.bp.blogspot.com/-6WNws4M97OY/WYHEVriXAYI/AAAAAAAAdPY/_eNoowXoXZ8kADmPLndEEVaOhvPnVk4aQCLcBGAs/s72-c/xDGJB0UUXoAAHCvv-750x375.jpg.pagespeed.ic.WqQj0SWivJ.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/08/mkojo-wa-wema-sepetu-wakutwa-una-bangi.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/08/mkojo-wa-wema-sepetu-wakutwa-una-bangi.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy