MNADA WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA YANGA WAKWAMA

Klabu bingwa ya ligi kuu ya Tanzania Bara, Young Africans, (Yanga) imepewa muda wa miezi mitatu kulipa deni la kodi ya ardhi inayodaiwa na serikali ili kunusuru kupigwa mnada kwa jengo la makao makuu ya klabu hiyo lililopo mtaa wa Jangwani, Dar es Salaam.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi aliizuia Kampuni ya Msolopa ya udalali kulipiga mnada jengo hilo la Yanga inayodaiwa kodi ya ardhi Tsh 360 milioni ambapo mnada huo ulikuwa ufanyike leo.
Hofu ilikuwa imetanda miongoni mwa wadau na mashabiki wa Yanga baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa serikali ingeliuza jengo hilo leo Agosti 19 ili kulipa malimbikizo hayo.
Wizara ya Ardhi ilisema jana kuwa ilisimamisha mnada huo baada ya kufikia makubaliano na  uongozi wa Yanga na kusaini mkataba kwamba watalipa fedha hizo ndani ya muda uliokubaliwa.
Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, alithibitisha kuwapo kwa deni hilo ambapo alisema deni hilo limetokana na malimbikizo ya ada ya jengo la kiwanja kinachomilikiwa na klabu hiyo.
Mkwasa alisema kuwa klabu hiyo inatakiwa kulipa kodi ya ardhi Tsh 56.6 kila mwaka.
Yanga inategemea kuanza kulipa deni hilo kwa mapato ya getini ambapo Bodi ya Ligi itakuwa ikikata 25% ya mapato ya Yanga kwenda serikali.
Kwa siku za hivi karibuni kumekuwapo na mgogoro wa kifedha ndani ya klabu ya Yanga ambapo baadhi ya wachezaji walidai kuwa hawakuwa wamelipwa mshahara kwa kipindi cha muda mrefu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post