MPIGA PICHA WA IKULU ATOA PICHA ALIZOZIPENDA ZA OBAMA KWA MWAKA 2016

Mpiga picha rasmi wa Ikulu katika utawala wa Rais Obama, Pete Souza, ametoa picha kadhaa za Rais Mstaafu Barack Obama alizopiga akiwa Ikulu ya nchi hiyo zikionesha matukio ambayo yalikuwa ni maisha ya kawaida kwa Rais huyo alipokuwa Ikulu. Hizi ni picha saba zilizopigwa mwaka 2016.

“Hivi ndivyo jinsi uandaaji wa hotuba kubwa ya Rais inapoanza, angalau kwa Rais Obama. Muda wa hutoba ukiwa umebaki mdogo, Rais aliwaita ofisini kwake Cody Keenan, Mkurugenzi wa Hotuba za Rais na Ben Rhodes, Kaimu Mshauri Mkuu wa Usalama wa Taifa kwa Mawasiliano Maalum na kuwasomea toleo la kwanza la hotuba yake.” Januari 7, 2016.


“Macho yangu yalitua kwa mtoto huyu wakati Rais Barack Obama alipokuwa akizungumza naye katika maadhimisho ya sherehe za Mwezi wa Wamarekani Weusi. Rais alipoanza kusamimia watu walio mstari wa mbele, niliinama na kupiga picha hii ya Rais alipomshika usoni kumsalimu. Baadae nilitafuta jina lake — Clark Reynolds — na nikampa Rais picha moja amsainie kwa ajili ya kumbukumbu yake ya baadae.” Februari 18, 2016.


“Jambo kubwa kuhusu watoto ni kwamba hujui watafanya nini watakapokuwa na Rais. Kwahiyo, David Axelrod akiwa na mmoja wa wajukuu zake, Maelin ambaye mara moja akapanda na kukaa kwenye kiti cha Makamu wa Rais huku Rais akiendeleza mazungumzo yake na watu waliokuwapo ofisini hapo. Muda huu, mtoto Maelin alikuwa akishangaa wakati Obama alipokuwa akiangalia vituko vyake.” Juni 22, 2016.


“Bill Murray alikuja Ikulu kupokea tuzo ya Mark Twain. Rais alipomfungulia mlango alicheka baada ya kumuona Bill akiwa amevaa nguo za klabu ya Chicago Cubs. Baada ya tuzo hizo, walirudi ofisini na kuanza kushindana kutumbukiza mpira wa gofu kwenye moja ya glasi za kunywea maji za Ikulu.” Oktoba 21, 2016.


“Rais Obama akimuangalia mkewe akicheza muziki na bibi mwenye miaka 106, Virginia McLaurin katika “Chumba cha Buluu” kwenye Ikulu ya Marekani kabla ya sherehe ya Mwezi wa Historia ya Wamarekani Weusi.” Februari 18, 2016.


“Ilitokea tu mchana mmoja tunamuaona Rais anacheza muziki na msaidizi wake Ferial Govashiri. Kwa kumbukumbu zangu, alikuwa akimsaidia kufanya mazoezi ya kujiandaa na harusi yake iliyokuwa karibuni.” Machi 16, 2016.


“Rais Obama mara nyingi alikuwa akiwaambia wafanyakazi wake wawalete watoto wao watembelee Ikulu. Hapa ilikuwa ni baada ya mkutano mchana mmoja ambapo Rais alikuwa anatambaa ofisini kwake pamoja na Vivi – mtoto wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu, Jen Psaki.” Aprili 14, 2016.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post