MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA AIGOMEA BARUA YA MAALIM SEIF YA KUWAVUA UANACHAMA WABUNGE WA CUF

Mgogogoro ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) bado unaendelea kufukuta baada ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kuwasilisha barua kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jon Ndugai akimtaarifu kuwa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF limewasimamisha uanachama wanachama wawili wa chama hicho ambao ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Magdalena Sakaya (Mbunge wa Kaliua) na Maftaha Nachuma (Mbunge wa Mtwara Mjini) uamuzi uliofikiwa kutokana na wajumbe wa mkutano huo kupiga kura za siri na kuamua kuwavua uanachama, hivyo kumuomba Spika Ndugai afanye utaratibu wa kuwavua ubunge wao kwa kuwa si wanachama halali wa chama hicho.
Baada ya barua hiyo, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amejibu barua ya Maalim Seif kwa kuwa kueleza kutomtambua yeye kama Katibu Mkuu wa CUF kwakuwa barua kutoka chama hicho ilisema kuwa nafasi ya Katibu Mkuu wa chama inakaimiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa haijapokea barua nyingine kutoka chama hicho ikionesha kumrejeshea Maalim Seif mamlaka yake.
Pia Jaji Mutungi amekataa matokeo ya kikao hicho kilichoitishwa na Maalim Seif kwakuwa kikao hicho kilitakiwa kiwe chini ya mtu mwenye dhamana ya Katibu Mkuu wa chama (Magdalena Sakaya) au Mwenyekiti wa CUF (ambaye ni Profesa Ibrahim Lipumba) na Jaji Mutungi akamkumbusha Maalim Seif arejee Katiba ya CUF ibara ya 91(c) inayotaka vikao vyote vya Baraza Kuu la chama hicho viongozwe na Mwenyekiti wa chama.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post