MSHINDI WA SUPER CUP KUPATIKANA LEO KATI YA BARCELONA NA REAL MADRID

Leo usiku, wababe wa ligi kuu ya soka nchini Hispania Barcelona na Real Madrid watashuka dimbani katika mpambano huo wa wapinzani wa jadi nchini Hispania unaojulikana kwa jina la utani la El Clásico. Mchezo wa leo utapigwa katika uwanja wa klabu ya Real Madrid (Santiago Bernabéu) baada ya mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye uwanja wa Camp Nou kuwania “Super Cup.”
Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Jumapili iliyopita, Real Madrid ilijizolea alama zote tatu kiaina yake ilipomaliza mchezo huo ikiwa na wachezaji kumi baada ya mshambuliaji wa kutegemewa wa timu hiyo, Cristiano Ronaldo kutolewa nje kwa kuoneshwa kadi nyekundu.
Kwa sasa, wachezaji wa nafasi ya kiungo ya Barcelona inatakiwa kufanya kazi ya ziada kwakuwa pengo la Neymar da Silva linaonekana wazi. Katika mchezo uliopita, Barcelona walionekana nyanya kwa kuzidiwa kabisa kwenye idara ya kiungo na kufanya Real kuwa na nafasi kubwa ya kuutawala mchezo pamoja na kufanya mashambulizi.
Barcelona inahitaji ushindi wa goli 4-2 au ushindi wowote wa zaidi ya goli tatu ili washinde kombe hilo, na kwakuwa wanahitajika kufunga magoli mengi – hii inaweza kuwa fursa kwa washambuliaji Gareth Bale na Karim Benzema kutaka kufunga zaidi kuongeza zaidi pengo hilo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post