MWANA FA: SIJAWAHI KUHONGA

Mwana FA.
RAPA asiyechuja kwenye muziki wa Hip Hop Bongo, Hamis Mwijuma ‘Mwana FA’ ametoa kali ya mwaka baada ya kusema kuwa katika maisha yake yote ya ujana, hajawahi kumhonga mwanamke pesa ili apendwe.
Akichonga na Risasi Vibes, Mwana FA alisema tabia ya kuhonga honga wanawake pesa na vitu vingine vya thamani ili kupendwa hilo kwake halijawahi kutokea tangu alipopata akili mpaka alipo sasa kwenye ndoa.
“Nihonge ili nipate nini, sijawahi kuhonga hata siku moja najua wengi wanaweza wasiamini lakini ndiyo hivyo, tabia hizo naishia kuziona kwa washkaji zangu huku mtaani lakini kwangu hazijawahi kuwepo maana kitendo hicho nakichukulia kama biashara ya kikahaba ambayo binafsi naichukia” alisema Mwana FA
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post