MWANAMUZIKI RUBY ATOBOA SIRI YA PENZI LAKE NA SOUDY BROWN

Baada ya kuishi kwa kujificha kwa miaka kadhaa, ubuyu wa mzee wa Shilawadu, Gossip Cop, Soudy Brown umeanikwa rasmi na mwanadada Ruby wa tasnia ya muziki wa kizazi kipya (Bongofleva). Mwanadada huyo ametoboa kwamba alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Mr. Shilawadu kwa zaidi ya miezi 18.
Kwa mujibu wa Ruby, uhusiano wao ulikuwa lazima ukatishwe kwa sababu Mzee wa Shilawadu alishindwa kabisa kujitolea kwenye uhusiano wao.
“Mwanaume pekee kwenye tasnia hii ambaye nishawahi kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi ni Soudy Brown lakini ilibidi tuachane kwa sababu hakuwa karibu nami katika kipindi nilichokuwa namhitaji,” aliiambia The Spin Tanzania.
Mwanamuziki huyo ambaye aligoma kushiriki kwenye matamasha ya Fiesta mwaka jana alisema kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki mwenzako ni kujitafutia maumivu ya kichwa kwa sababu wengi wao hawajatulia.
“Nimeona mambo mengi ambayo wasanii wa kiume wanavyowafanyia wapenzi wao. Kwa mfano unaweza kumuona mtu anamuacha mwanamke wake na kumfata msichana mwengine mchana kweupe! Hilo mimi siwezi kukubaliana nalo,” alisema.
Pamoja na kusema hayo, Ruby alikanusha tetesi kwamba alipata ujauzito katika uhusiano huo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post