MWANASHERIA WA TRUMP AMTISHIA MPELELEZI ANYETAKA KUCHUNGUZA BIASHARA ZA RAIS HUYO

Mwanasheria wa Rais Donald Trump wa Marekani, Jay Sekulow, ameliambia jarida la “The New Yorker” wiki hii kwamba timu ya wanasheria wa Rais huyo italichukulia kuwa ni kuvuka mipaka endapo Mpelelezi maalum wa Serikali, Robert Mueller ataamua kufanya upelelezi kuhusu ardhi aliyonunua Trump miaka sita iliyopita jijini Georgia akishirikiana na mmoja wa viongozi wa Kazakhstan ambaye ana uhusiano wa karibu sana na Rais wa Urusi, Vladimir Putin.
“Biashara tuliyoifanya jimboni Georgia ikiunganishwa na Urusi ni jambo ambalo sisi tutalioona lipo nje ya mipaka,” Sekulow aliliambia jarida hilo. “Jimbo la Georgia halipo Urusi, lipo Marekani.”
Alisema kwamba hatosita kupeleka malalamiko yake kea Makamu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Rod Rosenstein kama akigundua kwamba Mueller “anatoka” nje ya jambo la msingi la kuchunguza iwapo kulikuwa na “ushirikiano wowote kati ya Serikali ya Urusi na timu ya kampeni ya Trump.”
“Nataka kuwa muwazi tangu mwanzo,” alisema Mwanasheria huyo. “Kuchunguza biashara hiyo itakuwa ni kwenda nje ya uhitaji wa kisheria.” Hatutasita kwenda kwa Makamu Mwanasheria Mkuu ana mamlaka ya kumkataza Mueller pamoja na kusitisha upelelezi wake.
Rais Trump amekuwa akitishia kumfukuza kazi Mueller endapo atafanya upelelezi wake kuchunguza mambo yake ya biashara.
Biashara hii ya Trump jimboni Georgia ilikamilishwa na mmoja wa waliochangia fedha alikuwa ni Timur Kulibayev, ambaye ni mkwe wa Rais wa Kazakhstan ambaye alikuwa na jukumu la kusimamia utajiri wao katika benki ya B.T.A.
Benki hii ilikopesha baadhi ya kampuni zinazofanya kazi na kampuni zinazofanya kazi katika mradi huo wa Rais Trump jimboni Georgia, na Kulibayev huyohuyo alikuwa na uwezo wa kuwa na nyaraka zote za kibenki — ikimaanisha kuwa “alikuwa akiwajua vizuri watu wote waliohusika kwenye mradi huo,” liliandika jarida la The New Yorker. Kulibayev pia alikuwa akashiriki vikao vya bodi ya kampuni kubwa ya mafuta nchini Urusi, Gazprom, alikuwa na nafasi nzuri ya kupitisha taarifa yoyote itakayomdhuru Trump kwa maafisa wa Serikali ya Urusi.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post