MZEE MAJUTO: BADO NAUMWA JAMANI!

Mzee Majuto.
DAR ES SALAAM: Mungu tenda! Ikiwa ni siku chache tangu muigizaji mkongwe, Amri Athman Amri ‘King Majuto’kupata unafuu kufuatia upasuaji aliofanyiwa kutokana na tatizo la ugonjwa wa ngiri (hernia), hali yake bado haijatengemaa na anatumia muda mwingi kulala, Amani limezungumza naye kwa tabutabu.

Jumatatu ya wiki hii, mwandishi wetu alimpigia simu mzee huyo kwa lengo la kumjulia hali na kufanya naye mazungumzo mengine, lakini King Majuto alisikika kwa shida na kudai amelala na anahitaji muda mwingi wa kupumzika na kwamba bado anaumwa na anasikia maumivu makali.

Hata hivyo, mwandishi aliendelea kumdadisi kwa kina ili kujua ni nini hasa kinachoendelea kumsumbua kwani kama ni tatizo la awali alishafanyiwa upasuaji, ambapo aligoma kabisa kuendelea na mazungumzo na kugeuka ‘mbogo’ kwa muda kwa madai ya kutopenda mazungumzo na wanahabari.

“Bado nimelala jamani na sijui unataka nini tena? Naumwa na ninasikia maumivu sana na sitaki kuzungumza zaidi maana nimechoka, elewa tu kwamba bado naumwa na ningependa sana uniache ili nipate muda mwingi wa kupumzika, ni kweli hivi karibuni nilipata nafuu kabisa na kuanza kutembea lakini ndiyo hivyo bwana, bado hali haijakaa sawa,” alisema King Majuto.

TUKUMBUKE NYUMA KIDOGO!
Hivi karibuni, muigizaji huyo namba moja kwa sanaa ya vichekesho, aliripotiwa kuugua na kufanyiwa upasuaji wa ugonjwa wa ngiri (hernia) na kupata nafuu ambapo aliruhusiwa na hali yake kurejea kwenye utengamavu kabla ya mazungumzo ya habari hii, ingawa pia kulitokea na uzushi mwingi kwa watu wasiokuwa na kiasi katika mazungumzo, wakipotosha na kuvumisha uongo wa kuugua sana na hatimaye kifo, jambo ambalo King Majuto, ndugu na baadhi ya wadau wa sanaa walilikemea vikali.
STORI: BRIGHTON MASALU, AMANI
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post